Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yaanza 'kutetemeka' kileleni EPL

UBINGWA Pict

Muktasari:

  • Man City chini ya Pep Guardiola, imeonyesha uzoefu katika hatua za mwisho za msimu huku Arsenal wakikabiliwa na presha kubwa ya kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

LONDON, ENGLAND: VITA ya ubingwa wa Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2025-2026 imefikia hatua ya mwisho ambapo Arsenal na Manchester City sasa zimetenganishwa kwa tofauti ya pointi mbili huku zikiwa zimesalia mechi mbili kabla ya msimu kumalizika.

Kwa muda mrefu Arsenal ilionekana kuwa katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo lakini mwenendo wao wiki za mwisho umebadilisha hali ya mbio hizo na kuipa nafasi Manchester City ambao ushindi wa mabao 3-0 walioupata juzi Jumatano dhidi ya Crystal Palace umewafanya kufikisha pointi 77.

Man City chini ya Pep Guardiola, imeonyesha uzoefu katika hatua za mwisho za msimu huku Arsenal wakikabiliwa na presha kubwa ya kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

UBIN 01

Arsenal ambayo inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 79, sasa inakabiliwa na michezo miwili migumu ambayo inaweza kuamua hatima yao, mechi ya kwanza ni dhidi ya Burnley Mei 18 kwenye Uwanja wa Emirates, mchezo unaoonekana kuwa rahisi kwa macho ya wengi kutokana na nafasi ya Burnley kwenye msimamo wa ligi ikiwa tayari imeshuka daraja.

Hata hivyo, katika soka la England hakuna mchezo rahisi, hasa katika hatua ya mwisho ya msimu ambapo presha ya ubingwa inaweza kubadilisha kila kitu.

Katika mchezo wa awali wa msimu huu dhidi ya Burnley, Arsenal iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, mshambuliaji hatari wa kikosi hicho, Viktor Gyokeres alionesha kiwango bora kwa kufunga na kutoa asisti.

UBIN 02

Gyokeres sasa anatarajiwa kuwa moja ya silaha muhimu kwa Arsenal katika kuhakikisha inaendelea kusalia kileleni.

Arsenal inahitaji ushindi wa mechi hii ili kuweka presha kwa Man City kabla ya mchezo wa mwisho wa msimu.

Mechi ya pili ni ugenini dhidi ya Crystal Palace, Mei 24, mchezo ambao unaweza kutoa uamuzi wa moja kwa moja kuhusu ubingwa, Palace ikiwa nafasi ya katikati ya msimamo wa ligi, haina presha ya kushuka daraja lakini ina uwezo wa kuharibu mipango ya vigogo hao.

Kwa upande wa Man City, ratiba yao pia si nyepesi licha ya uzoefu wao mkubwa katika mbio za ubingwa.

Man City itasafiri kucheza dhidi ya Bournemouth Mei 19, mchezo unaoonekana kuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wao.

Bournemouth imekuwa katika kiwango kizuri msimu huu, ikicheza soka la kasi na nidhamu chini ya Andoni Iraola.

Imekuwa pia na mfululizo mzuri wa kutopoteza, jambo linaloifanya kuwa tishio kwa Man City katika safari ya ubingwa.

UBIN 03

Mechi ya mwisho ya Man City ni dhidi ya Aston Villa, Mei 24 katika uwanja wa nyumbani. Villa chini ya Unai Emery inapigania nafasi za kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, hivyo nayo itatolea macho mechi hiyo ili kupata matokeo mazuri.

Villa imewahi kuwa mpinzani mgumu kwa Man City katika misimu iliyopita, na inajua jinsi ya kukabiliana na vigogo wa ligi hiyo na katika mechi ya mwisho dhidi ya vijana hao wa Guardiola waliibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Matty Cash.