Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TB yafifisha matumaini ya mwanasoka John Ndirangu

Muktasari:

  • Bado anatumaini ingawa ni kidogo siku moja atarejea uwanjani na kufanya kile anachokipenda zaidi, kucheza soka. Kwa sasa anategemea watu wema na marafiki kwa ajili ya matunzo na dawa, na anawaomba wale wanaoweza kumsaidia kwa kazi yoyote ili kumsaidia kuishi.
  •  "Ninaamini mimi ni mtu ninayefanya kazi kwa bidii, mradi tu kazi siyo ya nguvu, naweza kuimudu," alisema.

LILIKUWA ni jambo la kuhuzunisha kama ilivyokuwa wazi mwanamume aliyeishi maisha yake yote akicheza mchezo alioupenda sasa anauacha na si kwa sababu alizozichagua mwenyewe, bali alilazimika kukabiliana na maisha yenye kutokuwa na uhakika.

Kwa mtu aliyekuwa akicheza soka la kiwango cha juu na timu kama vile Gor Mahia, AFC Leopards, Kenya Police, Kariobangi Sharks na Nakuru All Stars, John Ndirangu 'Softie' anajua vyema furaha inayokuja na mchezo huu mzuri na maumivu yanayokuja ya kujua hatoweza kucheza tena.

“Ni kwa machozi ninaposema hili. Sikuwahi kufikiria siku moja nitaachana na soka. Kutokana na hali yangu baada ya kuugua, siwezi tena kucheza. Labda huko mbele nitaweza. Mungu pekee anajua.

"Nimeamua kustaafu soka la kulipwa nikiwa na umri wa miaka 30. Napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wote walionisaidia kufikia mafanikio katika soka, wakala wangu na mlezi Robert Muthomi, kila kocha aliyenifundisha (Simon Mulama, Ezekiel Akwana na Francis Mwangi), pamoja na familia yangu na mashabiki wangu wote. Heshima kubwa. Kila hatua dua."

Huu ndio ujumbe wa hisia alioandika Ndirangu alipoitangazia dunia kuhusu kustaafu kwake soka Alhamisi iliyopita kutokana na mapambano marefu na ugonjwa wa kifua kikuu (TB) ambao umemfanya mwili wake kuwa dhaifu na daktari kumshauri kuepuka shughuli zozote zinazohitaji juhudi kubwa za kimwili, ikiwa ni pamoja na kucheza soka.

Ndirangu alizaliwa Septemba 27, 1995 katika Kaunti ya Nakuru na alianza kucheza soka akiwa Shuleni Kinari, kisha akaendelea na soka katika shule za Ngorika, Rohi na Spotlight Academy ambazo alisoma elimu ya sekondari.

Ndirangu amecheza katika winga zote mbili za kulia na kushoto pia akimudu kucheza kama kiungo mshambuliaji wa kati. Alicheza soka la kulipwa huko Dundori kabla ya kujiunga na Nakuru All Stars. Baadaye timu kubwa zilimuita.

Ndirangu anataja baadhi ya mafanikio yake katika soka ni kushinda ligi kuu Kenya akiwa na Gor Mahia mwaka 2017, kushinda Kombe la Super Cup huko Tanzania na kucheza dhidi ya timu ya EPL, Everton akiwa Gor.

"Nilikuwa nikiwaangalia wachezaji kama Christiano Ronaldo na Neymar na ndoto yangu kubwa ilikuwa ni kucheza katika majukwaa makubwa kama walivyokuwa wakifanya. Sasa ndoto hizo zimekuwa tu matamanio, lazima niache kazi yangu ya soka," amesema Ndirangu katika mahojiano aliyofanya na Nation Sport.

Amesema alianza kujisikia vibaya Julai iliyopita wakati mwili wake ulianza kuonyesha dalili za Pneumonia na TB lakini bila matokeo stahiki kila wakati vipimo vilipofanywa.

“Mapafu yangu yaliharibiwa na nikapata maumivu kwenye uti wa mgongo na miguuni. Katika hatua za awali sikuweza kupumua na kulazimika kutumia oksijeni kwa muda,” alisema.

Ameeleza daktari hakumshauri aache kucheza soka lakini anahisi mwili wake hauna nguvu za kutosha baada ya shida hiyo.

Bado anamatumaini ingawa ni kidogo siku moja atarejea uwanjani na kufanya kile anachokipenda zaidi, kucheza soka. Kwa sasa anategemea watu wema na marafiki kwa ajili ya matunzo na dawa, na anawaomba wale wanaoweza kumsaidia kwa kazi yoyote ili kumsaidia kuishi.

“Ninaamini mimi ni mtu anayefanya kazi kwa bidii na mradi tu kazi siyo ya nguvu, naweza kuimudu,” amesema.