Nyota Yanga Princess awasha moto Misri

Muktasari:
- Mwanzoni mwa msimu huu alitimkia Ligi ya Wanawake Misri na tayari amefunga mabao 25 nyuma ya vinara, Alice Ogebe wa FC Masar mwenye 27.
ALIYEKUWA mshambuliaji wa Yanga Princess, Mkenya Janet Bundi anayekipiga NBE FC ya Misri amezidi kung'ara akiwa kwenye tatu bora za wafungaji bora nchini humo.
Akiwa Yanga, alicheza nusu msimu akiingia dirisha dogo la msimu uliopita na kufunga mabao manne kwenye mechi tisa.
Mwanzoni mwa msimu huu alitimkia Ligi ya Wanawake Misri na tayari amefunga mabao 25 nyuma ya vinara, Alice Ogebe wa FC Masar mwenye 27.
Alipokuwa Yanga licha ya nafasi yake kutokuwa na ushindani mkubwa wa namba, alishindwa kuonyesha makali yake ya kufunga, lakini tangu ajiunge na ligi hiyo, amekuwa na kiwango bora jambo ambalo limefanya baadhi ya timu kubwa Misri kuanza kumfuatilia kupata saini yake.
Mabao yake yameisaidia NBE kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 41, nyuma ya vinara FC Masar (67 pointi), sawa na Al Ahly, Wadi Degla na Zamalek.