MULUMBA ADAI BANDARI HAKAI SANA, DILI IKIJIPA

Tuesday May 11 2021
bandari pic
By Thomas Matiko

NAHODHA wa Bandari, Felly Mulumba kasema hatasita kuihepa klabu hiyo tena ikitokea apate dili tamu kwingine.
Beki huyo kisiki aliwatoka Bandari Februari 2020 na kujiunga na Fc Platinum inayoshiriki ligi kuu ya Zambia.
Lakini baada ya mwaka mmoja huko Zambia, alivunja mkataba wake wa miaka miwili nao na kurejea tena Bandari aliokuwa amewahudumia kwa miaka mitano kabla ya kuondoka.
Sasa beki huyo wa Congo anasema bado tu anaweza kuondoka kama akipata ofa nzuri zaidi.
“Nipo tayari kuondoka ikiwa nitapokea ofa nzuri kwingineko. Isitoshe klabu pia itafaidi kutokana na uhamisho huo kwa namna moja au nyingine.” Mulumba anasema.
Hata hivyo Mulumba anasema anafurahia maisha yake huko Bandarini ambako kwa sasa anatumika zaidi kama kiungo mkabaji na kocha Mrwanda Casa Mbungo.
“Namshukuru kocha kwa kuamini uwezo wangu hata kwenye nafasi mpya hii. Sio mara ya kwanza mimi kucheza kama kiungo, niliwahi kucheza mid nilipokuwa na Sofapaka na Nakumatt vile vile.” Kaongeza.
Kando na kuwa beki na kiungo, Mulumba anachocha kuwa  hakuna safu asiyoweza kucheza uwanjani.
“Nimecheza kwenye nafasi nyingi tu. Nikiwa kulwe kwetu Congo niliwahi kuchezesha kama fulu-beki na pia straika. Ila nafasi yangu bomba kabisa ni beki wa kati.” Kaongeza.

Advertisement