Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi 410 FKF-PL hat-trick nne

LIGI Kuu Kenya itaingia mzunguko wa 24 mara tu baada ya mapumziko ya wiki mbili lakini takwimu za msimu huu zinaonyesha kati ya mechi 410 ambazo zimechezwa hadi sasa hat-trick nne tu ndizo zimeshuhudiwa.
Miongoni mwa wachezaji ambao walifunga mabao matatu katika mchezo moja ni straika raia wa Tanzania, Ibrahim Joshua, ambaye hivi karibuni aliitwa katika kikosi cha Taifa Stars nchini kwao kwa ajili ya mechi mbili za kimataifa za kirafiki.
Mechi hizo dhidi ya Sudan na Jamhuri ya Kati ambazo zimeandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa zintumika mahususi kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambaye ametimiza mwaka moja tangu kuapishwa.
Joshua aliyejiunga na Tusker FC akitokea Ken Gold FC ya nchini Tanzania, alifunga hat-trick katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mathare United ambapo moja ya mabao ilikuwa mkwaju wa penalti ya kusawazisha baada ya Clifford Alwanga kuipatia Mathare United bao la kuongoza.
Mchananyavu huyo ameshapachika mabao nane FKF-PL ikienda mapumziko akizidiwa mabao matatu na kinara wa mbio za Kiatu Cha Dhahabu, Yema Mwana, anayekipiga na Kakamega Homeboyz aliyojiunga nayo akitokea Bandari FC.
Joshua anamatumaini kibao ya kuibuka Mfungaji Bora katika msimu wake wa kwanza FKF-PL na pia kujihakikisha namba ya kudumu kikosi cha Taifa Stars kinachonolewa na Kim Poulsen.
“Ninamuomba Mungu anisaidia kutwaa Kiatu cha Dhahabu kwasababu hayo ndiyo malengo na nitapambana kupata mabao zaidi msimu huu. Kama straika ni kawaida ya kuwa na ndoto kushinda Kiatu cha Dhahabu kwasababu inaonyesha unafanya jambo sahihi,” alinukuliwa Joshua.
Levis Barasa ni straika mwingine aliyepiga hat-trick hadi sasa msimu huu katika mechi ambayo Nzoia Sugar iliifunga Kariobangi Sharks mabao 3-1.
Nzoia Sugar ipo katika nafasi ya 15 na pointi zake 25 ikimzidi kwa pointi tano Wazito FC iliyopo nafasi ya ‘playoff’ hivyo kutegemea zaidi mabao ya Barasa kuwaepusha rungu la kushuka daraja.
Kwenye orodha ya wachezaji waliyofunga hat-trick msimu huu yumo Felix Oluoch wa Kariobangi Sharks katika mechi ambayo timu yake iliigaragaza Mathare United mabao 6-0 huku Eric Mata akipachika mabao mengine mawili na moja likifungwa na Steve Otieno.
Straika Michael Isabwa kabla ya kutua Kakamega Homeboyz katika dirisha dogo, alifunga mabao matatu na kuisaidia iliyokuwa timu yake ya Vihiga Bullets kuichapa Wazito FC mabao 4-2.
Mbao hayo ya Isabwa na lingine lililofungwa na Vincent Onyango huku mabao ya Wazito FC yakipachikwa na Elli Asieche na Tyson Otieno yaliipa Vihiga Bullets inayofundishwa na Abdallah Juma ushindi wa kwanza baada ya mechi 13 za FKF-PL.