Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumekucha michuano iliyowaibua Fei Toto, Wanyama!

Muktasari:

  • Muktasari: Wanyama alishiriki mwaka 2004 na timu ya U-20 ya Mathare Youth Sports Association kutoka Nairobi,Feisal yeye alikuja na CHRISC Zanzibar mwaka 2013.

MICHUANO ya Vijana ya Afrika Mashariki (East Africa Cup) iliyowahi kuwaibua mastaa kama Feisal Salum na Victor Wanyama inatarajiwa kuanza kupigwa kwa muda wa wiki moja kati ya Juni 18-23 ikishirikisha zaidi ya timu 25.

Msimu wa 21 wa michuano hiyo tangu kuaisisiwa kwake, itafanyikia kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ufundi Moshi, yakiwa ni daraja kwa vijana wengi kutimiza ndoto zao kwani ikumbukwe.

Kiungo wa zamani wa Tottenham Hotspurs na Harambee  Stars, Victor Wanyama pamoja na staa wa Azam FC na  Taifa Stars, Feisal Salum 'Fei Toto' ni miongoni mwa waliowahi kushiriki michuano hiyo na kuwaka.

Wanyama alishiriki mwaka 2004 na timu ya U-20 ya Mathare Youth Sports Association kutoka Nairobi, huku Fei Toto alishiriki akiwa na CHRISC Zanzibar mwaka 2013. Wanyama kwa sasa amestaafu kucheza, huku Fei akiwa ni mmoja ya nyota walioiwezesha Azam kumaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara na kukata tiketi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu ujao ikiwa ni baada ya kupita miaka karibia 10.

Kiungo mshambuliaji huyo wa zamani wa JKU na Yanga amemaliza pia kama mfungaji wa pili katika Ligi Kuu akifunga 19 na kuasisti saba akiwa nyuma ya nyota wa Yanga, Stephane Aziz KI aliyefunga 21.

Msemaji wa michuano hiyo, Prisca Lema ameiambia Mwanaspotimaandalizi yanaendelea vyema na msimu huu zitashiriki zaidi ya timu 25 za  vijana wa kike na kiume wenye umri umri chini ya miaka 13-16.

Prisca ameongeza mbali na soka kutakuwa na michezo mingine kama Chesi na Kikapu ambapo pia washiriki wote watapata semina mbali mbali za stadi za maisha ambayo itawajenga na kuwafanya kutimiza ndoto zao zao.

“Mwaka huu tunaamini yatakuwa bora zaidi ya miaka yote kwani mwitikio umekuwa ni mkubwa lakini pia wapo mawakala ambao wameonyesha nia ya kuja kutafuta vipaji,” amesema Lema.