Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo wa boli aikacha Kenya ili akipige na Dube

FABISCH Pict

Muktasari:

  • Miongoni mwa mastaa wanaofanya vyema kwenye kikosi cha Zimbabwe kwenye mashindano ya Afcon 2025 ni Fabisch. Kiungo huyo anayecheza soka kwa akili kubwa alikuwa katika kiwango bora sana katika mechi dhidi ya Misri na Angola.

RABAT, MOROCCO: KIUNGO mzaliwa wa Kenya, Jonah Fabisch amefunguka uamuzi wake wa kuitumikia Zimbabwe kwenye soka la kimataifa na kuikacha Harambee Stars.

Miongoni mwa mastaa wanaofanya vyema kwenye kikosi cha Zimbabwe kwenye mashindano ya Afcon 2025 ni Fabisch. Kiungo huyo anayecheza soka kwa akili kubwa alikuwa katika kiwango bora sana katika mechi dhidi ya Misri na Angola.

Fabisch amekuwa kwenye kiwango bora akiwa na Zimbabwe, anayochezea pia staa wa Yanga, Prince Dube na hilo linaipa faida kubwa timu hiyo tofauti na nchi yake alikozaliwa.

Fabisch anatokea kwenye familia ya soka. Yeye ni mtoto wa marehemu Reinhard Fabisch, kocha wa Kijerumani, ambaye alikuwa na msaada mkubwa katika kulitengeneza soka la Zimbabwe na Kenya na amekuwa na hadhi kubwa kwenye Bara la Afrika.

FABIS 01

Reinhard Fabisch kwenye soka la kimataifa aliiongoza Harambee Stars kwenye fainali za All Africa Games 1987 zilizofanyika Kenya.

Kisha alikwenda kuinoa Zimbabwe kuanzia 1992 hadi 1994, kisha ikafuatia kuinoa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kabla ya kurudi tena Kenya. Reinhard alifariki dunia mwaka 2008 kwa maradhi ya saratani.

Na sasa, miaka 17 baadaye, jina lake linarudi tena kwenye soka, likipambwa na mwanaye, Jonah. Licha ya kwamba alikuwa na umri wa miaka saba wakati baba yake anafariki, kipaji cha soka bado hakikupoteza, kilifuata njia yake.

FABIS 02

Alizaliwa Kenya mwaka 2001 wakati baba yake alipokuwa kocha wa Harambee Stars kwa mara ya pili na Jonah alitumikia miezi ya mwanzoni baada ya kuzaliwa kwenye nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Alihamia Zimbabwe na baadaye Ujerumani na baba yake wakati mzee huyo alipokwenda kuinoa United Arab Emirates. Alikuwa na machaguo kadhaa kwenye kuitumikia timu ya taifa kati ya Kenya, Ujerumani na Zimbabwe, lakini kiungo huyo amechagua kuitumikia Zimbabwe, ambayo kwa sasa ipo kwenye mashindano ya Afcon 2025 huko Morocco.