Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Gor asare soka, maisha magumu

Nyota chipukizi kiungo wa Gor Mahia, Nicholas Omondi ameamua kuachana na mpira ili kusaka kazi inayoweza kumlisha.
Omondi ameahidi kurejea kwenye soka lakini kwa sasa anasema amelazimika kusare mpira sababu maisha ni magumu sana hasa ndani ya klabu hiyo inayozidi kuzongwa na ugumu wa kuwalipa mishahara wachezaji wake.
Kiungo huyo anasema haoni sababu ya kuendelea kupambana kuwa mchezaji wakati anashindwa kupata riziki ya kujikimu kimaisha na kwa maana hiyo ni bora asake kazi nyingine ya kufanya.
"Nimefurahia miaka niliyocheza soka na nataka kumshukuru kila mmoja aliyenishika mkono kwenye taaluma yangu. Lakini sasa nimeamua kuachana na mpira kwa sasa ili nikahangaikie maisha nje ya mpira. Baadhi ya maamuzi huwa magumu kufanya ila naamini huu ni uamuzi sahihi kwangu mimi" anasema chipukizi huyo wa miaka 19.
Aidha Omondi ameishtumu Gor kwa kumzibia njia yake ya kwenda kucheza soka la ki pro nje ya nchi.
"Pengine sasa hivi maisha yangu yangelikuwa tofauti kama Gor hawangenizibia njia yangu ya kwenda kucheza pro majuu. Nilihangaika sana kupata Visa na nikatumia fedha nyingi ila mwisho wa siku walinizuia kuondoka. Aidha pamoja na mimi kujituma sana uwanjani, klabu iliamua kuacha kuendelea kunilipa mshahara wangu, Omondi kadai.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Gor Lordovic Aduda anasisitiza kuwa hawajawahi kumzuia mchezaji yeyote aliyepata dili tamu nje ya klabu hiyo kuondoka.
"Tumewaaachia wachezaji wengi sana waliopata dili kwingine. Tuliwarahisishia stakabadhi zao wengine wakaishia Tanzania, Misri, na hata ngámbo sasa kwa nini tumnyime yeye barua ya kumwachia," Aduda kahoji.