Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kenya kwenye mtihani mzito uteuzi timu ya vijana

Vijana Pict

Muktasari:

  • The Starlets iliweka historia mwezi Oktoba mwaka jana kama timu ya kwanza ya taifa ya Kenya kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya umri wa miaka 17, mwaka 2024, zilizofanyika Jamhuri ya Dominica na walimaliza nafasi ya tatu katika Kundi 'C', wakishinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Mexico kwa 2-1.

Kocha wa timu ya soka ya wanawake ya Kenya chini ya miaka 17, Mildred Cheche ana kazi ya kujenga upya kikosi chake kabla ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia la Wanawake dhidi ya Uganda mwezi Machi.

The Starlets iliweka historia mwezi Oktoba mwaka jana kama timu ya kwanza ya taifa ya Kenya kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya umri wa miaka 17, mwaka 2024, zilizofanyika Jamhuri ya Dominica na walimaliza nafasi ya tatu katika Kundi 'C', wakishinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Mexico kwa 2-1.

Hata hivyo, wachezaji muhimu kutoka katika kikosi hicho tayari wamehamia kwenye timu ya Kenya chini ya umri wa miaka 20, hivyo kumlazimu Cheche kutafuta wachezaji wanaoweza kuchukua nafasi zao. 
Jana Jumatatu, kochahuyo anayemiliki Leseni ya CAF B alitangaza kikosi cha wachezaji 51 cha awali kwa ajili ya mchujo unaotarajiwa kufanyika Machi 7 na 16.

Miongoni mwa wachezaji waliopandishwa kwenye timu ya U-20 ni mabeki Diana Anyango na aliyekuwa nahodha Elizabeth Ochaka, pamoja na viungo Lorna Faith na Marion Serenge.

Licha ya mabadiliko hayo, baadhi ya wachezaji kutoka kikosi cha Jamhuri ya Dominica bado wanastahili kucheza, akiwemo kipa Velma Abwire na Scovia Awuor, mabeki Lorine Ilavonga na Jenevive Mithel, viungo Lindey Weey, Halima Imbachi, na Brenda Awuor, pamoja na washambuliaji Joy Valencia, Joan Ogola na Quinter Adhiambo.

“Kikosi kilichofuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia la U-17 kilichokuwa na wachezaji kama Lorna Faith, Marion Serenge, na Diana Anyango kilipandishwa kwenda timu ya U-20,” Cheche alikiri.

“Hii inafanya changamoto kuwa ngumu zaidi, lakini inawezekana. Uganda ni timu imara, tayari iko katika hali nzuri ya mchezo kutokana na kucheza katika raundi ya kwanza na tukiwashinda, mtihani mkubwa zaidi utakuwa dhidi ya Cameroon. Ili kujiandaa, tutacheza mechi kadhaa za kirafiki dhidi ya timu za hapa nyumbani. Lengo letu bado liko wazi, kufuzu kwa Kombe la Dunia la U-17, na tutatoa kila kitu kuhakikisha hilo linatimia.”

Tayari baadhi ya wachezaji wapya wamechaguliwa kutoka shule za msingi na sekondari, pamoja na klabu za Kenya na kipa Malia Rose Nyabera Otondi anayecheza Pelham Memorial ya New York, Marekani, ndiye mchezaji pekee wa kigeni katika kikosi hicho.

The Starlets inatarajiwa kuingia kambini wiki hii, huku mechi za kirafiki zikipangwa ili kuimarisha kikosi kabla ya kuivaa Uganda.

Uganda ilifuzu kwa raundi ya pili ya mchujo ya Kombe la Dunia la Wanawake la U-17 2025 kwa kishindo, ikishinda dhidi ya Namibia 10-1 na 8-1 katika raundi ya kwanza iliyofanyika mwezi Januari.