Infantino, Motsepe watua Kenya kushuhudia fainali ya CHAN 2024
Muktasari:
- Infantino amepokelewa na Rais wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) Hussein Mohamed mapema leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA.
Rais wa Shirikisho la Soka duniani (FIFA) Gianni Infantino akiambatana na Rais wa Shirirkisho la Soka Africa (CAF) Patrice Motsepe wamewasili Kenya alfajori ya leo kwaajili ya fainali ya CHAN 2024 kati ya Morocco na Madagascar utakaochezwa kwenye uwanja wa Moi Kasarani leo.
Infantino amepokewa na Rais wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) Hussein Mohamed mapema leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA.
Fainali hiyo itapigwa kuanzia saa 12:00 Jioni, huku msanii wa Bongo Fleva kutoka Tanzania Zuhura Otham Soud maarufu Zuchu akiwa miongoni mwa wasanii wataoipamba fainali hiyo.
- SAFARI YA MOROCCO, MADAGASCAR HADI KUFIKA FAINALI
MOROCCO
Matches 6
Wins 5
Draw 0
Lose 1
Goal Scored 10
Goal Conceded 4
Clean Sheets 2
MADAGASCAR
Matches 6
Wins 4
Draw 1
Lose 1
Goal Scored 7
Goal Conceded 4
Clean Sheets 3