Eti, waliosema Mashemeji Derby haifiki wako wapi?

RATIBA ya Ligi Kuu Kenya msimu 2023/24 ilipotoka, wengi waliuliza kwani Mashemeji Derby ni lini? Ni kama vile waliona hiyo siku haitafika au inakawaia kufika ila wahenga wanakwambia siku hazigandi.

Leo Jumamosi katika Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi, wakongwe wa soka la humu nchini wenye historia iliyotukuka ndani na nje ya mipaka ya Kenya, Gor Mahia na AFC Leopards wanakutana katika mchezo wa kwanza msimu huu wa FKFPL.

Leopards ndiyo watakuwa wenyeji wa mtanange huu ambapo wakati mwingi haijalishi fomu ya timu mbali ni namna gani wachezaji watakua wameamka siku hiyo. Huu sasa ndiyo utamu wa dabi.

Timu hizi mbili zinakutana zikiwa zimetenganishwa kwa pointi tano huku K’Ogalo wakiwa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa FKFPL na pointi tisa wakati Ingwe yenye pointi nne ipo nafasi ya 15.

Hii ni kumaanisha ushindi kwa Leopards utapunguza pengo lao la pointi na Gor Mahia hadi mbili na endapo Gor Mahia wataibuka kidedea watawaacha Leopards kwa pointi nane.
Mara ya mwisho timu hizi mbili kukutana ilikua ni katika mzunguko wa pili msimu uliyopita ambapo miongoni mwa waliyohudhuria gemu hiyo iliyopigwa Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, alikwepo Rais William Ruto na kiongozi wa Azimio la Umoja, Raila Odinga.

Watu wengine mashuhuri walikua Waziri wa Michezo Ababu Namwamba na mwenzake wa Madini Salim Mvurya, Mbunge wa Kasarani ambaye pia ni bosi wa SportPesa Ronald Karauri, Mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor aka Jalang’o na Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro.

Katika mechi hiyo, Ingwe walihitimisha ukame wa miaka saba ya kuwa wanyonge kila wanapokutana na K’Ogalo wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo mabao ya Leopards yalifungwa na Maxwell Otieno na Victor Omune huku lile la Gor Mahia likipachikwa na mchezaji wa zamani wa Ingwe, Austin Odhiambo.

Hivyo, kila timu inayo sababu ya kuwapa furaha mafans wake kwenye gemu ya leo inayotarajiwa kurushwa mubashara na Azam Media waliyoingia mkataba wa miaka saba na Shirikisho la Soka Kenya (FKF).

KWANINI INGWE WASHINDE
Ingwe chini ya ukufunzi wa mzawa Tom ‘Gazza’ Juma itakua inasaka ushindi wa ‘back-to-back’ kudhibitisha hawakuwafunga kwa fluki mabingwa watetezi wa FKFPL K’Ogalo walipokutana Mei mwaka huu.

Aidha ushindi kwa Leopards utaanzisha safari ya kuwatambia Gor Mahia wakilenga kulipiza miaka saba ya kushindwa kupata ushindi dhidi ya mashemeji zao.
Jinsi msimamo unavyosomeka kwasasa, ni sababu nyingine tosha ya Ingwe kuhakikisha baada ya dakika 90, wanaondoka na pointi zote tatu.

Timu hiyo ipo kwenye nafasi ya 15 na japo ni mapema mno katika mbio za ubingwa FKFPL msimu huu, hiyo sio nafasi ambao mafans wengi wangetarajia kuona timu yao kuwepo kutokana na usajili waliyofanya na maandalizi yao kabla ya msimu kuanza.

Kinachowasononesha mafans wa Ingwe ni kwamba hadi sasa katika michezo mitano, hawajapata ushindi na imani waliyonayo ni kwamba ushindi wa kwanza wa timu yao msimu huu itakua dhidi ya Gor Mahia.


KWANINI K’OGALO WASHINDE
Moja ya post za Gor Mahia kwenye mitandao ya kijamii kunogesha pambano hilo, lilikua na picha ya Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama, akitumia darubini kutazama kitu huku kukiwa na ujumbe uliyosomeka ‘admin akijaribu kutafuta ni lini walipoteza ‘back-to-back’ mchezo wa ligi dhidi ya Leopards’.
Hii ni kumaanisha K’Ogalo wataingia uwanjani kwa lengo la kulipiza kisasi kupoteza mchezo wao wa mwisho wa Mashemeji Derby.

Jambo lingine linalowasukuma Gor Mahia kusaka ushindi ni nia yao ya kutetea ubingwa wa FKFPL ambayo itawafanya kujiwekea historia ya kutwaa taji hilo mara 21 na kuzidi kuwaacha Leopards walioshinda ubingwa wa FKFPL mara 12.
Aidha K’Ogalo watataka kushinda gemu ya leo kuendelea kukimbizana na vinara wa ligi, Posta Rangers ambao kabla ya mechi ya jana Ijumaa dhidi ya Nzoia Sugar, walikuwa wamewazidi kwa pointi nne.

Kwa kocha Jonathan McKinstry ushindi ni muhimu kwasababu ndiyo itakuwa mara yake ya kwanza anaondoka na pointi tatu katika Mashemeji Derby baada ya kuambulia pointi moja tu kwenye sare tasa mzunguko wa kwanza msimu uliyopita.


HAT-TRICK MOJA TU
Historia inaonyesha Mashemeji Derby ya kwanza ilichezwa mwaka 1968 na Gor Mahia kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 nyota wa mchezo akiwa William Ouna ‘Chege’ aliyetupia kambani mabao wote mawili wakati Henry Misango akiifungia Leopards bao la pekee.

Lakini tangu mwaka huo, ni hat-trick moja imeshuhudiwa na japo kumekuwa na jitihada za kupatikana mchezaji anayefunga mabao matatu katika mechi moja, wachezaji hao wamekuwa wakiishia kufunga mabao mawili tu.
Listi ya wachezaji waliyofunga mabao mawili katika mechi moja ni kubwa hivyo Laban Otieno anabaki mchezaji pekee kupiga hat-trick katika Mashemeji Derby.

Straika huyo alifunga mabao hayo matatu mwaka 1975 katika mzunguko wa kwanza wa ligi na kuisaidia Gor Mahia kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 ikiwa pia ndiyo ushindi mkubwa kuwahi kushuhudiwa kwenye Mashemeji Derby.
Mabao mengine ya K’Ogalo katika mechi hiyo yalifungwa na Moris Ouma Ole Tunda na Francis Mudany wakati lile la kufutia machozi la Ingwe likipachikwa na Dennis Mwenje.


JAZA STADI
Ingwe na K’Ogalo zinajivunia utitiri wa mafans hivyo gemu ya leo ugani Moi Kasarani inatarajiwa kukusanya umati mkubwa ikiwezekana kuvunja rekodi ya msimu huu ya mashabiki kujaza uwanja iliyoshuhudiwa wikendi iliyopita wakati Leopards walipocheza na Shabana FC katika dimba la Ulinzi Sports Complex jijini Nairobi.

Leopards wamekuwa wakitumia mitandao yao ya kijamii kuwaita mafans uwanjani ikiwemo kuwaelekeza namna ya kukata tiketi ya mechi kwa mfumo wa kidigitali.
Naye kocha wa Gor Mahia McKinstry, amewahimiza wafuasi wa mabingwa hao wa kihistoria kujitokeza kwa wingi na kujaza Uwanja wa Moi Kasarani.

“Tutakuwa tayari kwa sababu hii ni gemu kubwa na tunatarajia umati utakua mkubwa ukizingatia Mashemeji Derby ni gemu special hivyo tujaze uwanja,” alisema kocha huyo raia wa Ireland Kaskazini.


DONDOO 6 MUHIMU
1. Zimepigwa mechi 92 za ligi hadi sasa ambapo Gor Mahia wameshinda mara 31 wakati Leopards wakiibuka kidedea mara 27 huku gemu 34 zikimalizika kwa sare.
2. Katika mechi hizo 92 za ligi, zimefungwa jumla ya mabao 165 huku Leopards wakiongoza kwa kupachika mabao 84 wakiwazidi kwa mabao matatu Gor Mahia.
3. Matokeo ya ushindi wa mabao 2-1 ndiyo yametawala zaidi baina ya miamba hii miwili takwimu zikionyesha mechi imeisha kwa matokeo ya aina hiyo mara 26.
4. Gemu tatu zimeshuhudia mabao ya kujifunga ambapo mwaka 1981 Hamisi Shamba wa Gor Mahia alijifunga, Allan Huma wa Leopards akajifunga timu hizo zilipokutana mwaka 2009 na mwaka 2017 Musa Mohammed wa Gor Mahia naye pia alijifunga.   
5. Ni wachezaji watatu tu; Abdul Baraza (Leopards), Dan Sserunkuma (Gor Mahia) na Meddie Kagere (Gor Mahia) wamefunga katika mechi tatu mfululizo za Mashemeji Derby.
6. Wachezaji ambao wameshafunga wakichezea timu hizo mbili katika nyakati tofauti ni David Deo Odhiambo na Demonde Selenga.


 

MASHEMEJI WALIVYOKUTANA GEMU ZA LIGI
1968 - 1st leg
Leopards 1 (Henry Misango)
Gor Mahia 2 (William Ouna ‘Chege’-2)

1968 - 2nd leg
Gor Mahia 1 (Chris Obure)
Leopards 1 (Noah Wanyama)

1969 - Hamna ligi

1970 - 1st leg tu
Leopards 1 (David Asibwa)
Gor Mahia 0

1971 - 1st leg tu
Leopards 1 (Jonathan Niva)
Gor Mahia 1 (Dennis Olando)

1972 - Walishiriki ligi tofauti

1973 - 1st leg
Walishiriki makundi tofauti hadi raundi ya pili

1973 - 2nd leg
Leopards 2 (David Asibwa-2)
Gor Mahia 1 (Dennis Olando)

1974 - Leopards walisusia ligi

1975 - 1st leg
Leopards 1 (Dennis Mwenje)
Gor Mahia 5 (Laban Otieno-3, Morris Ouma Ole Tunda, Francis Mudany)

1975 - 2nd leg
Leopards 1 (Aggrey Lukoye)
Gor Mahia 0

1976 - 1st leg
Leopards 1 (Timothy Madonye)
Gor Mahia 2 (Maurice Ochieng, George Yoga)

1976 - 2nd leg
Leopards 0
Gor Mahia 1 (Francis Mudany)

1977 - 1st leg
Leopards 1 (Aggrey Lukoye)
Gor Mahia 1 (Maurice Ochieng)

1977 - 2nd leg
Leopards 1 (Patrick Okumu)
Gor Mahia 1 (Maurice Ochieng)

1978 - 1st leg
Leopards 2 (Abdul Baraza, Maltus Akello)
Gor Mahia 1 (Paul Oduwo 'Cobra')

1978 - 2nd leg
Leopards 1 (Abdul Baraza)
Gor Mahia 0

1979 - 1st leg
Leopards 1 (Abdul Baraza)
Gor Mahia 2 (Nahashon Oluoch, Jerry Imbo)

1979 - 2nd leg
Leopards 2 (Johannes Ndombi, Paul Maungu)
Gor Mahia 0

1980 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

1980- 2nd leg
Leopards 0
Gor Mahia 1 (Andrew Obunga)

1981 - 1st leg
Leopards 3 (Joe Masiga-2, Hamis Shamba-OG)
Gor Mahia 1 (Sammy Owino)

1981 - 2nd leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

1982 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

1982 - 2nd leg
Leopards 0
Gor Mahia 1 (Sammy Onyango)

1983 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

1983 - 2nd leg
Leopards 0
Gor Mahia 1 (Sammy Onyango)

1984 - 1st leg
Leopards 1 (Moses Mulumba)
Gor Mahia 0

1984 - 2nd leg
Leopards 2 (Wilberforce Mulamba-2)
Gor Mahia 1 (Sammy Onyango)


1985 - 1st leg
Leopards 1 (Francis Kadenge)
Gor Mahia 2 (Abbas Magongo-2)


1986 - 1st leg
Leopards 2 (Mike Amwayi, Dabid Akon)
Gor Mahia 1 (Sammy Onyango)


1986 - 2nd leg
Leopards 3 (Dan Musuku-2, Patrick Shim)
Gor Mahia 2 (Sammy Onyango-2)

 
1987 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 1 (Peter Dawo)


1987 - 2nd leg
Leopards 2 (Francis Kadenge, John Shoto Lukoye)
Gor Mahia 2 (Hezron Osuka-2)

1988 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

1988 - 2nd leg
Leopards 1 (Wilberforce Mulamba)
Gor Mahia 1 (Peter Dawo)

1989 - 1st leg
Leopards 1 (John Shoto Lukoye)
Gor Mahia 1 (Peter Dawo)

1989 - 2nd leg
Leopards 0
Gor Mahia 1 (George Odembo Nyangi)

1990 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

1990 - 2nd leg
Leopards 1 (Ben Gachie)
Gor Mahia 0

1991 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 1 (Paul Ochieng)

1991 - 2nd leg
Leopards 2 (Tony Lwanga, Kitali Ngaira)
Gor Mahia 1 (Tom Odhiambo)

1992 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 1 (David Odhiambo 'Deo')

1992 - 2nd leg
Leopards 1 (Kitali Ngaira)
Gor Mahia 1 (Dan Ogada)

1993 - 1st leg
Leopards 1 (John Odie)
Gor Mahia 2 (James Atuto, Allan Odhiambo)

1993 - 2nd leg
Leopards 1 (John Odie)
Gor Mahia 0

1994 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

1994 - 2nd leg
Leopards 2 (Francis Oduor, John Odie)
Gor Mahia 0

1995 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

 
1995 - 2nd leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

1996 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

1996 - 2nd leg
Leopards 2 (David Odhiambo, Joseph Weke)
Gor Mahia 1 (Dan Ogada)

 
1997 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

 
1997 - 2nd leg
Leopards 0
Gor Mahia 1 (Steve Okumu)

 
1998 - 1st leg
Leopards 2 (Fred Ambani, Philip Ouma)
Gor Mahia 0


1998 - 2nd leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

 
1999 - 1st leg
Leopards 1 (Philip Ouma)
Gor Mahia 0

 
1999 - 2nd leg
Leopards 3 (George Waweru, Fred Ambani, Ben Makuto)
Gor Mahia 0

2000 - Walikuwa makundi tofauti

2001 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

 
2001 - 2nd leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

2002 - Walikuwa makundi tofauti


2003 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

2003 - 2nd leg
Leopards 3 (Dickson Amalo, Ramadhan Balala, Ahmed Farid)
Gor Mahia 2 (Patrick Oyiengo, Emmnauel Wakata)

2004 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 1 (Ken Oliech)


2004 - 2nd leg
Leopards 1 (Wafula Mwanda)
Gor Mahia 0


2005 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 1 (Ken Oliech)

 
2005 - 2nd leg
Gor Mahia waliingia mitini ikabidi Leopards wapewe walkover ya mabao 2-0


2006 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

 
2006 - 2nd leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

2007/2008 - Leopards walishushwa daraja

 
2009 - 1st leg
Leopards 2 (Francis Xavier-2)
Gor Mahia 3 (Allan Huma-OG, Zablon Otieno, Habil Otieno)

 
2009 - 2nd leg
Leopards 1 (Obadiah Ndege)
Gor Mahia 0

 
2010 - 1st leg
Leopards 1 (Demonde Selenga)
Gor Mahia 0

 
2010 - 2nd leg
Leopards 0
Gor Mahia 1 (Collins Okoth)

 
2011 - 1st leg
Leopards 1 (Mike Barasa)
Gor Mahia 3 (Wycliff Ochomo, Demonde Selenga, Dan Makori)

2011 - 2nd leg
Leopards 3 (Charles Okwemba, Mike Barasa, Laurent Tumba)
Gor Mahia 0

 
2012 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

2012 - 2nd leg
Leopards 1 (Mike Barasa)
Gor Mahia 2 (Dan Sserunkuma-2)

 
2013 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 1 (Dan Sserunkuma)

2013 - 2nd leg
Leopards 2 (Noah Wafula, Paul Were)
Gor Mahia 2 (Dan Sserunkuma, David Owino)

 
2014 - 1st leg
Leopards 3 (Jacob Keli, Charles Okwemba, Bernard Mangoli)
Gor Mahia 1 (Timonah Wafula)

 
2014 - 2nd leg
Gor Mahia 2 (Dan Sserunkuma-2)
Leopards 2 (Noah Wafula, Martin Imbalambala)

2015 - 1st leg
Leopards 1 (Jacob Keli)
Gor Mahia 1 (Ali Abondo)

 
2015 - 2nd leg
Mafans wa Leopards wafanya vurugu hivyo Gor Mahia wapewa ushindi wa mabao 2-0

 
2016 - 1st leg
Leopards 1 (Lamin Diallo)
Gor Mahia 0

 
2016 - 2nd leg
Leopards 0
Gor Mahia 2 (Meddie Kagere, Enock Agwanda)

 
2017 - 1st leg
Gor Mahia 3 (Meddie Kagere, George Odhiambo, Timothy Otieno)
Leopards 0

 
2017 - 2nd leg
Leopards 1 (Musa Mohammed-OG)
Gor Mahia 1 (Meddie Kagere)


2018 - 1st leg
Leopards 1 (Wyvonne Isuza )
Gor Mahia 2 (Jacques Tuyisenge, George Odhiambo)

 
2018 - 2nd leg
Gor Mahia 2 (Boniface Omondi, Bernard Ondiek)
Leopards 0


2018/19 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 2 (Francis Kahata, Kenneth Muguna)

2018/19 - 2nd leg
Gor Mahia 3 (Nicholas Kipkirui-2, Jacques Tuyisenge)
Leopards 1 (Vincent Oburu)

 
2019/20 - 1st leg
Leopards 1 (Tresor Ndikumana)
Gor Mahia 4 (Gnamien Yikpe-2, Clifton Miheso, Lawrence Juma)

 
2019/20 - 2nd leg
Gor Mahia 1 (Boniface Omondi)
Leopards 0

 
2020/21 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0

 
2020/21 - 2nd leg
Leopards 0
Gor Mahia 1 (Boniface Omondi)


2021/22 - 1st leg
Gor Mahia 1 (Benson Omalla)
Leopards 1 (Victor Omune)

 
2021/22 - 2nd leg
Leopards 1 (Collins Shivachi)
Gor Mahia 1 (Austin Odhiambo)

 
2022/23 - 1st leg
Leopards 0
Gor Mahia 0