Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Asikwambia mtu maze kuna raha yake mbio ubingwa NSL

USHINDANI uliopo ubingwa wa Ligi Kuu Kenya hususan kati ya Tusker FC na Gor Mahia, hautofautiani na ule unaoshuhudiwa Supaligi ya Taifa (NSL) kati ya Shabana FC na Murang’a Seal.
Hata hivyo kilichodhahiri ni kuwa wageni wapya FKFPL msimu ujao watatoka nje ya jiji la Nairobi lakini je, kati ya timu hizo mbili; Murang’a Seal na Shabana FC, nani ataibuka bingwa NSL?
Kanuni za uendeshaji soka humu nchini chini ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF) zinabainisha timu mbili za juu NSL zinafuzu moja kwa moja kukipiga FKFPL msimu ujao huku inayoshika nafasi ya tatu ikicheza playoff na timu inayomaliza nafasi ya 16 FKFPL.

Migori Youth FC na Mara Sugar zote zikiwa na pointi 50 zinatolea macho nafasi ya tatu ili kucheza playoff huku Silibwet Leons, Vihiga United na Kajiado zikipambana kuepuka rungu la kushuka daraja.

SHABANA WAITAKA TENA
Mara ya mwisho Shabana FC kushiriki ligi ngazi ya juu nchini ilikuwa mwaka 2006 ambapo walishushwa daraja pamoja na miamba AFC Leopards na Kisumu Telkom iliyokuwa ikifahamika kama Kisumu Posta.
Wakati Shabana FC inashushwa daraja, Sony Sugar yenye maskani yake Awendo kaunti ya Migori chini ya kocha Francis Baraza iliweka historia kuwa timu ya kwanza kutoka kanda ya ziwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Kenya.
Shabana FC imekuwa katika fomu bomba msimu huu ikishiriki NSL na wapo mbioni kurudi tena FKFPL baada ya kukaa gizani kwa miaka 17 lakini kocha Sam Okoth anawatahadharisha wachezaji wake wasilaze damu.
Ushindani mkubwa hadi sasa unatoka kwa Murang’a Seal FC ambao wameingia wikendi hii wakiwa kileleni kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Naivas gemu iliyopigwa katikati ya wiki.
Kocha Okoth alinukuliwa akisema japo wapo katika nafasi nzuri kutwaa ubingwa NSL ukizingatia bado wana mechi mbili mkononi huku wakihitaji ushindi gemu tatu kati ya sita walizobakisha, ni mapema mno kuanza kusherehekea.
“Unakumbuka nini kilichowatokea Arsenal wiki chache zilizopita walipodhani wameshinda ubingwa wa ligi England na badala yake wakaishia kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo? Hivyo ndivyo msimu unavyoweza kubadilika kwa sekunde chache,” alitahadharisha Okoth ambaye mwaka 2020 aliiongoza Vihiga United kupanda daraja kukipiga FKFPL.
Msimu huu kwenye NSL, takwimu zinaonyesha Shabana FC ndiyo inaongoza kuwa na mafans loyal wanaojitokeza kwa wingi hususan gemu za nyumbani na kuipa sapoti vijana wao ambapo wamepoteza mchezo moja kati ya 13 walizocheza Uwanja wa Gusii, Kaunti ya Kisii.

MURANG’A SEAL WAKOMAA
Anayemfukuza Shabana FC kimya kimya ubingwa wa NSL ni Murang’a Seal chini ya ukufunzi wa Vincent Nyaberi ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea Shabana FC.
Nusura aiongoze Murang’a Seal kukipiga FKFPL msimu uliopita, lakini walipoteza mchezo wa playoff dhidi ya Wazito FC na hata kama wangeshinda wasingeshiriki ligi hiyo baada ya FKF kuufuta msimu wa 2021/22.
Nyaberi alisema watapambana hadi dakika ya mwisho kutimiza lengo lao la kutwaa ubingwa NSL na hii ni baada ya mabao ya aliyekuwa straika wa Gor Mahia, John Kiplangat na Fabian Adikiny, kuipa Murang’a Seal ushindi dhidi ya Naivas na kuwapiku Shabana FC kileleni.
“Kwetu sisi sasa, kila gemu ni fainali. Hakuna timu rahisi na ninataka nihimize vijana wangu kuendelea kupambana katika mechi nne za mwisho. Tutapambana hadi siku ya mwisho kwasababu huwezi kujua, hata Shabana wanaweza kudondosha pointi,” alisema kocha wa Murang’a Seal.

MIHELA FORTUNE YAYEYUKA
Maamuzi ya FKF kuifuta msimu wa 2021/22 yaliiumiza sana klabu ya Fortune Sacco ambayo ilikua imefuzu kukipiga FKFPL kufuatia kumaliza nafasi ya pili NSL.
Laiti ligi hiyo ambayo wakati huo ilisimamiwa na Kamati Shirikishi FKF isingefutwa, mafans kutoka Kaunti ya Kirinyanga wangepata burudani ya FKFPL.
Fortune Sacco FC walirudishwa kucheza NSL lakini FKF ikawapiga rungu ya kuwashusha zaidi hadi Ligi Divisheni ya Kwanza kwa kushindwa kucheza mechi hata moja mwanzoni mwa msimu wa 2022/23.
Timu hii ambayo ipo chini ya udhamini wa Fortune Sacco ilipata pigo zaidi baada ya mdhamini kudhibitisha uamuzi wa kuivunjilia mbali na kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu Fortune Sacco, Timothy Muthike, mambo yalibadilika kwasababu walihisi hamna tena haja kushiriki ligi ngazi ya chini ambayo haikuwa matarajio yao.
“Hatuna tena msisimko, furaha ya kufuzu haipo tena na maisha yameendelea,” alinukuliwa Muthike na kuongeza mdhamini alikua tayari kutoa mamilioni ya fedha kugharamia mahitaji ya timu kwa msimu mzima.
“Tulikua tumetenga Sh12 milioni kwa ajili ya msimu huu lakini mfadhili akashindwa kutoa fedha baada Fortune Sacco FC kukataliwa kucheza FKFPL.

APS BOMET INAUMA
Kama ilivyokuwa kwa Fortune Sacco FC ndivyo ilivyokuwa kwa Administration Police Bomet ambao ndoto yao kukipiga FKFPL ilikwamishwa na uamuzi wa FKF kuufuta msimu uliopita.
APS Bomet waliyokuwa mabingwa NSL msimu wa 2021/22 waliwasilisha malalamiko yao kwa Tume ya Usuluhishi wa Michezo (SDT) wakitaka kuorodheshwa kwenye ratiba ya FKFPL msimu huu wa 2022/23 lakini FKF wakashikilia kidete warudi tena kucheza NSL.
Timu hiyo iliyosusia kucheza mechi za NSL ilishushwa hadi Ligi Daraja la Kwanza baada ya shirikisho kutumia kanuni za uendeshaji soka nchini za mwaka 2019 kuwahukumu.
“Tunataka tuwatarifu kuwa APS Bomet FC imesimamishwa kushiriki NSL msimu wa 2022/23 na kushushwa hadi Ligi Daraja la Kwanza msimu 2023/24,” ilisomeka taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Doris Petra mapema mwaka huu wakati huo akiwa Kaimu Rais FKF.