Ambani, Juma hatushuki msimu huu

Ikiwa zimesalia mechi tano Ligi Kuu ya wanaume ya FKFPL msimu huu wa 2021/22 kukamilika timu ya Wazito Fc na Vihiga Bullets zipo taabani kushuka daraja .
Kocha wa timu ya Wazito Fred Ambani na kocha Wa Vihiga Bullets Abdallah Juma ,wakizungumza na Mwanaspoti kuhusiana na kushuka daraja msimu huu kila mmoja alionekana kuwa na imani ya kusalia Ligi Kuu .
Mechi ya awali dhidi ya Wazito Fc na Nairobi city Stars katika uga wa Kasarani Annex siku ya Jumatatu Wazito walilala mikononi mwa City Stars kwa kwa bao 1-0 .
Kocha Ambani, alinyoosha kidole cha lawama kwa mwamuzi wa mechi hiyo ambaye alionekana kuegemea upande mmoja kwa kupeana penalti ambayo haikuwa inastahiki.
“Ikiwa Kila wikendi marefarii watakuwa wakifanya maamuzi ambayo haya stahili tunapocheza na timu yoyote , hii itaendelea kutuweka  kwenye hatari zaidi .Tunafanya mazoezi Kila siku ilituwe bora zaidi lakini wanaharibu mchezo wetu mzuri , nitakacho ahidi ni kuwa ikiwa marefa watafanya maamuzi mazuri wakati wa mechi zetu nina imani kuwa mechi zilizosalia tutashinda  zote na tutoke kwenye hatari.” Alikiri Ambani
Kwa upande wa kocha mwenzake wa timu ya Vihiga Abdallah Juma anasema tangu ujio wake kwenye timu hiyo amenyoosha mambo na anastahili kutuzwa kuwa kocha bora msimu huu .
“Vijana wanacheza vizuri na hii ni kutokana na kujituma vizuri mzoezini, jinsi wanacheza tunaeza tukapigana na kujiondea kwenye hatari ya kushuka daraja nina imani tunaweza. Mechi zilizosalia dhidi ya Bandari, Ulinzi Stars, Sofapaka, Wazito na Police Fc zote tutashinda Ligi hii hatutoki," alisisitiza Juma
Kwenye mechi ya awali waliandikisha ushindi wa 4-3 dhidi ya Kariobangi Sharks katika uga wa Kasarani Annex siku ya Jumapili.
Vihiga kwa sasa wameshikilia nafasi ya 16 na alama 23 baada ya kupiga ushindi Mara Sita ,sare nane na kupoteza mechi 15, Wazito nao nafasi 17 na alama 22 wamepiga ushindi Mara tano, sare saba na kupoteza mechi 17 .Mathare United wapo mkiani na alama 18.