Zamalek kukiwasha Azam

MABINGWA wa Ligi Kuu mara 20 ya nchini Misri Zamalek FC wanatarajiwa kutua jijini Dar es Salaam wiki hii kwaajili ya kuikabili klabu ya Flambeau du Centre ya Burundi katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumamosi kwenye uwanja wa Azam Complex huku wenyeji wa mchezo huo Flambeau du Centre nao wanatarijiwa kutua nchini siku za hivi karibuni.

Awali klabu hizo zilifikia makubaliano ya kucheza mechi zao zote mbili  nchini Misri.


Hata hivyo mabingwa hao wa Burundi hautakuwa mchezo wao wa kwanza kwenye Uwanja wa Azam Complex kwani mechi yao dhidi ya Al Attihad ya Libya walicheza kwenye uwanja huo ambapo waliibuka na ushindi wa bao 1-0.