Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yatia mkono dili la kiungo Simba

DILI Pict

LICHA ya Yanga kufanikisha kumuongeza mkataba mpya kiungo Khalid Aucho ili aendelea kuitumikia timu hiyo, inadaiwa mabosi wa Jangwani wameamua kutia mkono katika dili la kiungo mmoja fundi wa mpira kutoka klabu ya Cs Sfaxien aliyekuwa akiwindwa na Simba.


Lengo la Yanga kutaka kumvuta kiungo huyo ni kumuongezea nguvu Aucho, lakini akishikilia pia hatma ya Dube Abuya ambaye anacheza pia katika nafasi hiyo kuendelea kusalia kikosini au la.


Ipo hivi. Balla Moussa Conte anayekipiga CS Sfaxien ya Tunisia, alikuwa anatajwa kuwa katika mazungumzo na Simba ni kama watani zao Yanga wameingilia kati dili hilo na wameonyesha nia uhitaji zaidi kutokana na kutuma ofa ya kumhitaji klabu anayoitumia kwa sasa.

Simba na Yanga zote zimekuwa zikielezwa kusaka kiungo mkabaji ili kuweka mambo sawa na uwezo wa Conte ilionekana katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika, wakati Simba ikishinda bao 1-0 mbele ya wenyeji hao, ambapo nyota huyo alikiwasha eneo la kati licha ya chama lao kupoteza nyumbani.hiyo.

Mwanaspoti lilisharipoti kuwa kiungo huyo anatakiwa na Simba baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kwenye mchezo dhidi yao Yanga pia imeingilia dili hilo kwa kuonyesha nia ya kumuhitaji mchezaji huyo.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kimeliambia Mwanaspoti kuwa hili ni dirisha la usajili timu yenye fedha ndio inaweza kukamilisha dili bila kujali mchezaji anawaniwa na timu ngapi.

"Hakuna mchezaji wa timu fulani mchezaji anaweza kucheza timu yeyote kwa makubaliano ya pande zote mbili hivyo ni suala la muda kujua mchezaji huyo ataitumikia timu gani msimu ujao," alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza;

"Yanga inaongezwa nguvu kutokana na aina wachezaji waliopo kikosini malengo ni kuwa bora zaidi ya msimu uliopita na kuweza kufikia mafanikio ya kufanya vizuri Ligi ya Mabigwa Afrika usajili tunaofanya ni kutengeneza timu bora zaidi ya msimu uliopita tukizingatia ndani na kimataifa."

Mtoa taarifa huyo pia alizungumzia suala la kiungo Duke Abuya kuwa makubaliano ya kumuongeza mkataba mpya bado hayajafikiwa na endapo watamuongeza watampeleka Singida Black Stars kwa mkopo ili kupisha usajili mpya.

"Ni kweli kuna wachezaji wawili wa kigeni eneo la kiungo mkabaji Duke na Aucho lakini ni mmoja tu ambaye ameongeza mkataba mpya huku mwingine mazungumzo yakiwa yanaendelea licha ya kutokuwa sehemu ya kikosi endapo tutakamilisha dili la Conte."

Chanzo hicho kilisema wanahofia kumpoteza Duke kabla ya kukamilisha usajili mpya hivyo kwa sasa wanaendelea kukaa naye kwa mazungumzo huku wakipambania mchakato wa kumpata Conte ambaye wanaamini ataongeza chachu ya ushindani kikosini mwao.