Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yashusha kitasa kipya, msaidizi wa Aucho

Muktasari:

  • Kiungo huyo amejiunga na Yanga kuongeza nguvu eneo la kiungo cha ukabaji ambapo anaungana na Khalid Aucho na Jonas Mkude.

KLABU ya Yanga imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji, Aziz Andambwile kutoka Singida Fountain Gates kwa mkataba wa miaka miwili.

Kiungo huyo amejiunga na Yanga kuongeza nguvu eneo la kiungo cha ukabaji ambapo anaungana na Khalid Aucho na Jonas Mkude.

Usajili wa kiungo huyo unamaanisha kwamba anakwenda kuchukua nafasi ya Zawadi Mauya ambaye hivi karibuni aliondoka baada ya mkataba wake kumalizika akiwa ameitumikia timu hiyo kwa miaka minne kuanzia 2020 hadi 2024.

Andambwile anakuwa mchezaji wa tano mpya kutambulishwa ndani ya Yanga kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa baada ya Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka na Khomeiny Aboubakar.