Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yanunua kijanja mechi tatu kali Simba

Kikosi cha Yanga kikifanya mazoezi magumu jijini Dar es Salaam siku za hivi karibuni

MWANDISHI WETU SARE ya bao 1-1 baina Yanga na Mgambo JKT Jumatano iliyopita imezidi kuiweka pabaya Azam kwani urafiki wa mashaka baina ya Simba na Yanga utaendelea mpaka Mei Mosi wakati ambao Mnyama atakuwa amecheza mechi tatu na kufaidi mashabiki wa bure kutoka Jangwani. Wanachama matajiri wenye ushawishi mkubwa Yanga wamezidi kuwachochea mashabiki wao kuizomea Azam na kuipa sapoti Simba (kama kejeli) kwavile wanadhani kuendelea kufanya vizuri kwa Azam kwenye ligi ya ndani na michuano ya kimataifa kutaipa nguvu na kuuweka rehani ubingwa wa Yanga. Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata kutoka ndani ya Yanga ni kwamba wataendelea kuisapoti Simba kinafiki mpaka watakapotwaa ubingwa kwenye mechi dhidi ya Coastal Union mjini Tanga Mei Mosi. Hiyo inamaanisha kwamba Yanga itakuwa imeisapoti Simba kwenye mechi tatu ambazo ni ile iliyopita dhidi ya Azam walipotoa sare ya 2-2, ijayo dhidi ya Ruvu Shooting Aprili 25 na nyingine dhidi ya Polisi Morogoro Aprili 28 zote zikichezwa Dar es Salaam. Mmoja wa vinara wa kampeni hiyo ambaye ana ushawishi mkubwa kwa wanachama na mashabiki alidai kuwa kwa kuisapoti Simba, Yanga itakuwa na nguvu pia kwenye mechi ya Coastal mjini Tanga ambayo ni ngumu kutokana na rekodi za sare za Yanga mikoani. "Tukishinda mechi na Ruvu Shooting Jumapili (kesho) na ile ya Coastal tutakuwa mabingwa hivyo hatutakuwa na shida tena na Azam. Simba tukiwa nao karibu watatusapoti pia kwenye mechi ya Coastal kule Tanga ambayo ni ngumu." Yanga inahitaji pointi nne kutwaa ubingwa wa Bara kwani itakuwa imefikisha pointi 57 ambazo Azam walioko nafasi ya pili hata wakishinda mechi tatu wataishia pointi 56. Viongozi waliopo madarakani Yanga wamesita kutoa tamko rasmi kwa madai kuwa ni mambo ya mashabiki tu. Kocha wa Azam, Sterwart Hall amesisitiza kuwa hawawezi kuzuia muungano wa mashabiki wa Simba na Yanga ila watakachofanya ni kucheza soka safi na kulenga zaidi kushinda na kuchukua pointi iwe kwenye Kombe la Shirikisho au ligi ya ndani: "Wana uhuru wa kufanya wanachofanya si juu yetu."