Yanga yamtimua Zlatko

Muktasari:

Uongozi wa Yanga umemfukuza kazi kocha mkuu wa Yanga, Zlatico Krmpotick baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa siku 35.

Uongozi wa Yanga umemfukuza kazi kocha mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotick baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa siku 35.

Mserbia huyo aliwasili Dar es Salaam Agosti 29 na kutambulishwa rasmi Agosti 30, 2020 kwenye kilele cha maazimisho ya Siku ya Wananchi

Taarifa ya klabu iliyotolewa jana usiku imesema kuwa klabu hiyo imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kocha huyo.

"Uongozi wa Klabu ya Yanga unapenda kuwataarifu mashabiki, wapeni na wanachama wa Yanga kuwa Klabu imefikia makubaliano na Mwalimu Zlatko Krmpotick ya kusitisha mkataba wake mara moja" imesema taarifa hiyo bila kutoa sababu za kuachana naye

Taarifa hiyo iliyosainiwa na kaimu Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Wakili Simon Patrick imekuja baada ya Wanajangwani kupata ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Costal Union, ushindi ambao ni mkubwa kwa Yanga tangu msimu huu uanze.

Katika taarifa hiyo, haijabainisha utaratibu wa kumpata kocha mwingine

Katika mechi tano za Ligi kuu Bara ambazo Yanga imecheza, wameshinda mivhezo minne na kutoka sare mchezo mmoja.

Awali katika mchakato wa kumpata kocha mkuu wa kuinoa timu hiyo kabla ya msimu huu kuanza, Yanga ilimtaja Mrundi, Cedrick Kaze kuwa kocha mkuu lakini wakati akitarajiwa kutua nchini, klabu hiyo ikaeleza kuachana naye baada ya kocha huyo kuomba udhuru wa wiki mbili na ikamtaja Krmpotic kuwa kocha mkuu.

Zlatko alijiunga na Wanajangwani hao kuchukua nafasi ya Kocha mkuu wa Luc Eymael ambaye naye alitimuliwa