Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yamtambulisha mrithi wa Nabi

Muktasari:

  • Kocha huyo raia wa Argentina ametambulishwa leo na Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ally Kamwe wakati wa mkutano mkuu unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).

KLABU ya Yanga imemtambulisha rasmi Kocha Mkuu, Miguel Angel Gamondi kuinoa timu hiyo msimu ujao akichukua nafasi ya Nasreddine Nabi aliyemaliza mkataba wake.

Kocha huyo raia wa Argentina ametambulishwa leo na Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ally Kamwe wakati wa mkutano mkuu unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).

Gomondi mwenye uzoefu na soka la Afrika kwa zaidi ya miaka 20 amewahi kuzifundisha timu mbalimbali ikiwemo USM Alger ya Algeria, Mamelodi Sundown (Afrika Kusini) na Wydad Casablanca kutoka nchini Morocco.

Hii ni mara ya pili kwa Yanga kutoa surprise (mshangao) kwa wanachama wake katika mkutano wao kwani Julai mwaka jana ilimtambulisha kiungo wa Burundi, Gael Bigirimana aliyewahi kucheza Newcastle ya England.