Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mossi amfunika Sowah Singida BS

Muktasari:

  • Mossi ameonyesha kiwango cha juu katika hatua za mwisho za msimu ambapo amefunga mabao matano ndani ya mechi mbili zilizopita.

KIUNGO mshambuliaji wa Singida Black Stars, Mossi Nduwumwe ameendelea kuandika historia ndani ya kikosi hicho baada ya kuvunja rekodi iliyowekwa na mshambuliaji wa Ghana, Jonathan Sowah, kufuatia kufikisha mabao 14 katika Ligi Kuu Bara msimu huu.

Mossi ameonyesha kiwango cha juu katika hatua za mwisho za msimu ambapo amefunga mabao matano ndani ya mechi mbili zilizopita.

Nyota huyo alitikisa nyavu mara tatu (hat trick) katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Dodoma Jiji kabla ya kuongeza mabao mawili mengine kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tanzania Prisons.

Mabao hayo yameifanya Singida Black Stars kuendelea kupambana kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara huku Mossi akigeuka kuwa mchezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Mabao hayo yamemfanya Mossi kumpiku Sowah ambaye alimaliza msimu wa 2024/25 akiwa na mabao 13 ya Ligi Kuu Bara akiwa na Singida Black Stars ambayo alitua wakati wa dirisha dogo la usajili la Januari 2025 akitokea klabu ya Al Nasr ya Libya. Sowah alifikisha idadi hiyo ya mabao ndani ya mechi 14 pekee na kuweka alama iliyodhaniwa kuwa ngumu kufikiwa.

Hata hivyo, Mossi ambaye alitua Singida Black Stars Januari 2026 akitokea Flambeau CFC ya Burundi, ameonyesha kuwa ni moto wa kuotea mbali kwa kuvunja rekodi hiyo akiwa bado amebakiza mechi mbili za ligi dhidi ya Simba SC na Fountain Gate FC.

Akizungumza kuhusu mafanikio hayo, Mossi alisema anafurahishwa na kiwango anachoendelea kukionyesha lakini akaeleza kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano wa wachezaji wenzake na benchi la ufundi.

"Ninafurahi kuona juhudi zangu zinaleta matokeo mazuri. Kuvunja rekodi ni jambo kubwa kwangu lakini muhimu zaidi ni kuisaidia timu kupata ushindi. Wachezaji wenzangu na makocha wamekuwa na mchango mkubwa katika mabao haya. Bado hatujamaliza kazi kwa sababu tuna mechi mbili muhimu mbele yetu," alisema nyota huyo.

Mossi alisema malengo yake si tu kuongeza idadi ya mabao bali kuhakikisha Singida Black Stars inamaliza msimu katika nafasi nzuri na kufikia malengo iliyojiwekea.

"Kila mchezo ninaingia uwanjani nikiwa na nia ya kusaidia timu. Nikifunga ni ziada lakini kikubwa ni ushindi wa timu. Natumaini nitaendelea na kiwango hiki hadi mwisho wa msimu," alisema nyota huyo mwenye idadi sawa na kinara wa ufungaji Ligi Kuu Bara, Feisal Salum.

Kwa sasa, Mossi amejiweka katika nafasi nzuri ya kumaliza msimu akiwa miongoni mwa wafungaji bora wa Ligi Kuu Bara, huku akithibitisha kuwa usajili wake kutoka Flambeau CFC ulikuwa moja ya uamuzi bora yaliyofanywa na Singida Black Stars katika dirisha la Januari.