Yanga yamshtua Brigamana wa Stand United

Muktasari:

  • Straika Blaise Brigimana amejikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya kuandamwa na jinamizi la kadi akiwa na kikosi chake cha Stand United

KOCHA Amars Niyongabo wa Stand United, ameamua kufunguka kwamba imebidi wafanye kazi ya ziada kuhakikisha kwamba mchezaji wao Blaise Brigimana anaweza kuepukana na upataji wa kadi ovyo uliomuandama hivi saa.
Brigimana alipata kadi tatu za njano tatu zilizomfanya akose mchezo dhidi ya Yanga, lakini alirejea na kucheza dhidi ya KMC na Ndanda kisha akapata kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Mbeya City.
Akizungumza na Mwanaspoti, Niyongabo alisema kwamba mchezaji wake mabeki wamejua yupo katika hali gani pindi anapokuwa na hasira hivyo humchokoza ili kumtoa mchezoni.
“Blaise ni mchezaji mzuri na kila mmoja anafahamu hilo, lakini kinachotokea ni kwamba mabeki wanamfanyia makusudi makosa na anapokuwa uwanjani akirudisha anapata kadi yeye,” alisema.
Aliongeza hali hiyo imekuwa ikiwagharimu kama timu, hivyo alikaa na mchezaji huyo ili kuhakikisha suala hilo linaenda vizuri na lisijirudie.