Yanga yaendeleza ubabe kwa Simba, Mayele aiteka shoo

Yanga yaendeleza ubabe kwa Simba, Mayele aiteka shoo

Yanga imeendeleza ubabe wake mbele ya Simba kwenye Ngao ya Jamii kwa mara pili mfululizo kwa ushindi wa mabao 2-1 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mabao mawili ya mshambuliaji Fiston Mayele yameiwezesha Yanga kutoka nyuma baada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa Simba kwenda mapumziko ikiongoza bao 1-0.
Tangu kipindi cha pili kianze Yanga imeonekana kutumia vizuri maeneo yake ya pembeni ambako kuna wachezaji walioingia kipindi cha pili, Jesus Moloko na Bernard Morrison.

Injini inayoonekana kuwaka Azizi Ki inonekana kutawala eneo la juu ya kiungo cha Yanga kuwabidi kucheza soka la kwenda mbele zaidi.

Simba inacheza pasi chache kwenda mbele, licha ya mabadiliko kadhaa kufanywa na Zoran ikiwemo kuingia Mzamiru Yassin, John Bocco na Nelson Okwa  yanonekana kushindwa kufua dafu.

Mabao mawili yaliyofungwa na Mayele yametosha kuamsha vaibu kwa mshabiki wa Yanga huku Simba wakinyong'onyea.