Yanga yaandika rekodi mpya Bara ikiichapa Coastal

Muktasari:
- Awali Yanga ilikuwa inashikilia rekodi hiyo sawa na Matajiri wa Chamazi Azam FC ya kucheza mechi 38 bila kupoteza ambapo Azam ilifanya hivyo kati ya Feb 23, 2013 hadi Oktoba 25, 2014 huku Yanga ikiweka rekodi hiyo kati ya Mei 15, 2021 hadi leo Agosti 16, 2022 kabla ya leo kuandika rekodi mpya.
Klabu ya Yanga imeandika rekodi mpya Ligi Kuu Bara ya kucheza mechi 39 bila kupoteza baada ya kuifunga Coastal Union mabao 2-0 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Timu hiyo msimu uliopita 2021/22 ilichukua Ubingwa wa Ligi Kuu NBC bila kupoteza mechi hata moja ilizocheza za ligi na na kuanza msimu kwa ushindi wa mechi zake mbili na kufanya kufikia idadi hiyo.
Awali Yanga ilikuwa inashikilia rekodi hiyo sawa na Matajiri wa Chamazi Azam FC ya kucheza mechi 38 bila kupoteza ambapo Azam ilifanya hivyo kati ya Feb 23, 2013 hadi Oktoba 25, 2014 huku Yanga ikiweka rekodi hiyo kati ya Mei 15, 2021 hadi leo Agosti 16, 2022 kabla ya leo kuandika rekodi mpya.
Katika mchezo wa leo dhidi ya Coastal ilichukua Dakika 4 tu za mchezo kabla mchezaji wa Yanga Bernard Morrison kufungua dimba kwa bao la kwanza baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Jesus Moloko.
Katika mchezo huo, Dakika ya 55 alitoka Makambo na kuingia mshambuliaji tegemezi wa Yanga Fiston Mayele aliyechangamsha mchezo na kupelekea dakika ya 68 kupata bao la pili kwa kupiga kichwa mpira uliorudishwa kwenye eneo la hatari na beki Shaban Djuma.
Katika mchezo huo kadi za njano zilitawala ambapo dakika ya 12 wachezaji Mtenje Albano alizawadiwa kadi ya njano baada ya kumkanyaga Yanick Bangala aliyejibu mapigo kwa kumsukuma mchezaji huyo naye akaambulia kadi hiyo hiyo.
Dakika ya 32 mchezeshaji wa Yanga Morrison nae ameonyeshwa kadi ya njano kwa kosa la kutaka kumhadaa mwamuzi kwa kujiangusha eneo la hatari.
Dakika ya 53 Aucho alipewa kadi ya njano na kuifanya Yanga kuvuna kadi ya tatu ya njano baada ya kumchezea madhambi Mtenje Albano wa Coast na Dakika ya 62 kocha msaidizi wa Yanga Cedric Kaze akipaonyeshwa kadi nyingine baada ya kusimama na kuonyesha hasira kwa kupiga kopo la maji teke.
Dakika ya 64 Nimubona wa Coastal alipewa kadi ya njano na kufanya timu hiyo kuwa na kadi mbili katika mchezo huo.
Mabadiliko ya Yanga walitoka Moloko, Morrison , Azizi ki, Kibwana huku wakangia Farid Mussa, Dickson Ambundo, Mayele, na Malissa
Mabadiliko ya coastal Union walitoka Betrand, Gerald, Mubakari, Vicent huku wakangia Saimon, William, Hamad, Mbaruku
Kikosi Cha Yanga kilichoanza golini yuko Abutwalib Mshery, Djuma Shaban, Kibwana Shomari Yanick Bangala, Bakri Nondo, Feisal Salum, Khalid Aucho, Bernard Morrison, Jesus Moloko, Aziz Ki na Heritier Makambo.
Waliobaki benchi wakiwa ni Fiston Mayele, Farid Mussa Dickson Ambundo,Lomalisa, Job, Bigirimana na Bacca.
Kikosi cha Coastal Union kilichoanza ni Kipa Mahamud, Nimubona, Miraj, Khatibu, Lameck, Mtenje, Vicent, Betrand, Maabad, Greyson, moubarack
Huku waliobaki benchi ni Mohamed, Omary, Jackson, Joseph, Gustaph, Pembele , Hamad, Willium, Opatatus