Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga wanajiamini vizuri, hawapangiwi

Muktasari:

Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema; “Hakuna wasiwasi kwanza mashabiki wanatakiwa kufahamu Yanga inapokuwa ugenini inacheza mpira mzuri kuliko hapa nyumbani ndiyo maana nasema tutafanikiwa na hata hizo figisufigisu za nje ya uwanja tutapambana nazo kwa sababu mpira unachezwa uwanjani.”

KOCHA wa Yanga, George Lwandamina amesisitiza kwamba hana hofu yoyote, na kwenye mechi ya marudiano dhidi ya MC Alger Jumamosi atacheza soka la kushambulia ila kwa tahadhari kubwa. Katika mechi ya kwanza Yanga ilishinda bao 1-0 Taifa.

Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema; “Hakuna wasiwasi kwanza mashabiki wanatakiwa kufahamu Yanga inapokuwa ugenini inacheza mpira mzuri kuliko hapa nyumbani ndiyo maana nasema tutafanikiwa na hata hizo figisufigisu za nje ya uwanja tutapambana nazo kwa sababu mpira unachezwa uwanjani.”

Cannavaro ambaye ni mchezaji mwenye miaka mingi zaidi ndani ya klabu hiyo tangu ajiunge 2006 anasema hawana wasiwasi kwani amegundua wakiwa ugenini wanafanya vizuri zaidi kwavile hakuna kelele za Simba ambao wanawakejeli zao uwanja wa Taifa.

KAULI YA LWANDAMINA

“Tumewaona na tunawafanyia kazi na kujadiliana ili mechi ya marudiano iwe nzuri kwetu na inawezekana kabisa kuwafunga hukohuko kwao. MC Alger ni timu nzuri lakini pamoja na ushindi wa bao moja tulionao tutakwenda kushambulia na kupata ushindi mwingine na pia tutahakikisha haturuhusu goli la kufungwa,”alisema Lwandamina ambaye kwa kawaida siyo muongeaji.

WAARABU WALIA

Afisa Mtendaji Mkuu wa MC Alger alisema jana mjini Algiers kwamba; “Matokeo ya kufungwa bao 1-0 siyo mabaya, tulitaka kufunga lakini hatukufanya hivyo. Tutafunga tukiwa kwetu.”

Kiongozi huyo alilalamika walipofika kwenye Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam Yanga hawakuwapa usafiri lakini akadai kuwa wao hawatalipiza. “Tutawapokea vizuri, tutawaonyesha kwamba Algeria ni sehemu rafiki kwa wageni. Lakini ndani ya Uwanja ndiyo tutawaonyesha kazi,” alisema.