Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipa azigonganisha Simba, Yanga

Picha kwa msaada wa AI


SIMBA, Yanga na Singida Black Stars zimeingia vitani kuisaka saini ya kipa wa Pamba, Yona Amosi, ambaye kwa sasa ni moja wa makipa bora zaidi katika Ligi Kuu Bara.


Tangu alipotua Pamba Jiji akitokea Tanzania Prisons msimu uliopita, Yona amekuwa katika kiwango bora kilichofanya mara kadhaa aitwe katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.


REKODI ZINAMBEBA

Ikumbukwe kuwa, kipa huyo ndiyo kinara wa kuokoa michomo ‘saves’ msimu wa 2024/25 kiwango ambacho amekiendeleza msimu huu akiwa anaongoza pia hadi sasa wakati zimebakia mechi tano za Ligi Kuu Bara. Katika msimu wake wa kwanza (2024/25), alionyesha kiwango kikubwa na kufanikiwa kucheza mechi 11 bila kuruhusu nyavu zake kuguswa (clean sheets). Rekodi hii ilimfanya kuwa kipa wa pili mzawa mwenye clean sheets nyingi msimu huo nyuma ya Patrick Munthali. Clean sheets za msimu huu (2025/26). Hadi kufikia sasa, ameshafanikiwa kuzifikia clean sheets 7 akipambana kuvunja au kufikia rekodi yake ya msimu uliopita.


KILICHOWAVUTIA SIMBA

Simba inataka kuimalisha eneo la kipa msimu ujao hasa baada ya makipa wake wote mikataba yao itafika tamati mwisho wa msimu. Kipa Hussein Abel mkataba wake utafikia tamati mwishoni mwa msimu huu, lakini si hivyo tu Yakoub Suleiman ni majeruhi atakuwa nje kwa nusu ya msimu ujao kutokana na majeraha. Wakati Simba ikiendelea kupiga hesabu za kipa gani wa kigeni wanaenda naye msimu ujao kati ya Djibrilla Kassali au Moussa Camara, wanataka kuhakikisha wanajaza nafasi ya eneo hilo kwa wazawa mwenye kiwango cha juu ndipo jina la Yona linajitokeza.


YANGA MMOJA OUT

Jangwani nako pa moto kwani hatma ya kipa Abubakar Khomeni bado inautata kwani inadaiwa kuwa kiwango chake hakijawaridhisha mabosi wa klabu hiyo, huku mkataba wake ukielekea ukingoni.

Mbali ya Khomeni, Masalanga ameshindwa kuonyesha ushindani kwa Aboutwalib Mshery na Djigui Diarra hivyo uwepo wa Yona utaongeza ushindani kwa makipa hao.


SINGIDA HATUA MOJA

Singida Black Stars ndio timu ya kwanza kuonyesha nia kwa kipa huyo, huku taarifa za ndani zilieleza kuwa tayari wamempa Yona mkataba wa miaka miwili.

“Ni kweli Singida BS wamempa mkataba wa miaka miwili, lakini bado hajatia saini. Simba na Yanga pia wametuma ofa zao na sasa anaendelea kuzichambua kabla ya kufanya uamuzi,”  kilisema chanzo hicho.

Kiongozi mmoja wa Singida ambaye hakutaka kutajwa alisema ;”Tunahitaji kupata kipa mwenye muendelezo wa kiwango chake, hili ni eneo ambalo kwetu bado halikuwa na utulivu, hesabu zetu zipo kwa Yona,”.