Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga vs Mbao...

DAKIKA 45 KIPINDI CHA KWANZA

>Rahael Daudi anaipatia Yanga bao la kuongoza dakika ya 16'

>Dakika ya 44' mabao Yanga 1-0 Mbao

>Dakika zimeongezwa 2'

>DAKIKA 45 kipindi cha kwanza timu zinakwenda mapumziko Yanga ikiwa inaongoza bao 1-0 dhidi ya Mbao FC

DONDOO MUHIMU NA MWANDISHI THOMAS NG'ITU


TIMU ya Yanga imeanza kuliona lango la Mbao FC dakika 16 baada ya kiungo Raphael Daud kuweka mpira wavuni.

Daud aliweka wavuni baada ya Ibrahim Ajib kupiga krosi na Daud kuionganisha kwa kichwa.

Katika mchezo huo Mbao walianza kwa kushambulia langoni mwa Yanga, hata hivyo mabeki wa Yanga walionyesha utulivu.

Goli hilo ni kama liliwaamsha Yanga kwani walianza kucheza kwa madoido na kuonyesha soka safi.

Dakika 22 Mbao walifanya mashambulizi mfululizo ya piga nikupige lakini mabeki wa Yanga waliutoa mpira na kuwa kona isiyokuwa na faida.

>>>>>>

Yanga  na Mbao FC zinacheza muda huu usiku ambapo  tangu ipande msimu wa 2016-2017 timu hiyo ya Kanda ya Ziwa, haijawahi kupata ushindi kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya wapinzani wao hao, ingawa inapochezwa CCM Kirumba haijawahi kupoteza kwa Yanga katika michuano yoyote kwamba kila mmoja mbabe kwake.

Mbao iliifunga Yanga katika mechi ya robo fainali ya Kombe la FA misimu miwili iliyopita kabla ya kutibua sherehe za ubingwa kwa klabu hiyo kwa kuwachapa siku chache baadaye msimu wao wa kwanza wa Ligi Kuu.

Msimu uliopita walirudia tena kuwatia adabu Yanga kwa kuwacharaza mabao 2-0 pale Kirumba, ingawa mechi zote za ugenini jijini Dar kwa misimu hiyo miwili ilipoteza kwa mabao 3-0 na 1-0.