Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga treni imechanganya

YANGA haizuiliki tena. Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara wameendelea kuthibitisha kuwa wamejipanga vilivyo katika michuano ya kombe la Mapinduzi, baada ya jana jioni kuichapata JKU bao 1-0 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Bao la kideo la Hassan Kessy katika dakika ya 89 lilitosha kuwatuliza mabingwa hao wa Zanzibar ambao walitandaza kandanda safi tangu mwanzo wa mchezo lakini hawakuwa na umakini katika umaliziaji.

Gumzo kubwa katika bao la Yanga ni pasi ya kisigino ya Pius Buswita ambaye amezidi kuwa mtamu klabuni hapo. Kessy aliwakimbiza mabeki wa JKU na kisha kumpasia Buswita aliyepiga kisigino kilichomkuta tena Kessy kwenye eneo la kufunga na kufuta unyonge huo.

Yanga sasa imefikisha pointi sita sawa na Singida United, lakini inashika nafasi ya pili kwenye kundi lake kutokana na kuzidiwa mabao ya kufunga na kufungwa. Singida imefunga mabao sita na kufungwa matatu wakati Yanga imefunga matatu na kufungwa moja.

Licha ya Yanga kuanza mchezo wa jana na mastaa wake karibu wote, JKU walionekana kutawala katika nafasi ya kati huku kiungo wao Feisal Salum ‘Toto’ aking’ara na kumpoteza kabisa Pappy Kabamba Tshishimbi. Yanga ilimtoa Matteo Antony na kumpa nafasi Yohana Mkomola katika kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko kwa kuwatoa Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Juma Mahadhi na nafasi zao zilizibwa na Raphael Daud na Said Mussa. Baadaye waliwatoa Emmanuel Martin na Tshishimbi na kuwapa nafasi Ibrahim Ajibu na Geofrey Mwashiuya.

Baada ya kufanya mabadiliko hayo, Yanga walionekana kuimarika katika nafasi ya kiungo lakini bado JKU walifanya mashambulizi mengi ambayo hata hivyo hayakuweza kuwapa bao.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kessy alikiri wapinzani wao walikuwa wazuri, lakini Mungu aliwasaidia na kuwapa ushindi.

“JKU wanacheza vizuri, tunashukuru kwamba tumeshinda mchezo. Kwetu tulifuata zaidi kile ambacho benchi la ufundi lilitaka tufanye,” alisema Kessy.

“Michezo ya hapa imefatana sana, hivyo wachezaji na benchi la ufundi tunatakiwa kushikamana na kupambana,” alisisitiza Kessy ambaye kwenye Ligi Kuu amekuwa akipata nafasi ndogo ya kucheza.

Yanga inarejea uwanjani leo Ijumaa usiku kucheza na Taifa Jang’ombe kabla ya Jumatatu kumalizia mechi yake ya mwisho ya hatua ya makundi dhidi ya Singida United.