Yanga kucheza bila mashabiki

Thursday September 09 2021
mashabiki pic
By Mwandishi Wetu

RASMI sasa mechi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Rivers United itapigwa bila mashabiki kwenye uwanja wa Mkapa, Dar.

Kama ilivyokuwa kwa Taifa Stars dhidi ya Madagascar mashabiki hawakuruhusiwa kutokana na tahadhari za ugonjwa wa corona sasa Wananchi watashuhudia mechi hiyo wakiwa majumbani.

Mmoja wa viongozi wa Yanga ameithibitishia Mwanaspoti taarifa hiyo ambayo ilikuwa inasubiriwa na mashabiki wa soka nchini akisema mpaka sasa hawajaruhusiwa kuingiza mashabiki ingawa bado wanaendelea kuomba Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Wawakilishi wengine wa kimataifa Azam FC nao watawakosa mashabiki wao wakati wakiikaribisha Horseed Jumamosi Septemba 11 mechi ya Kombe la Shirikisho.


KWA TAARIFA ZAIDI SOMA GAZETI LA MWANASPOTI IJUMAA SEPTEMBA 10, 2021 KUJUA VIONGOZI WA TIMU ZOTE WAMESEMAJE

Advertisement
Advertisement