Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga hii sasa sifa...Mayele, Saido watakata

Yanga hii sasa sifa...Mayele, Saido watakata

Vinara wa Ligi Kuu Bara Yanga, wameendeleza moto wao baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0, dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Mkapa.
Katika mchezo huo mabao ya Yanga yalifungwa na Fiston Mayele aliyeweka kambani mawili na lingine alifunga Saido Ntibazonkiza.
Mabao mawili ya Mayele yanamfanya kufikisha jumla ya mabao tisa moja nyuma ya kinara wa ufungaji Reliant Lusajo wa Namungo.
Wakati Saido amefikisha mabao sita na kutoa pasi za mwisho tano kumfanya kuhusika katika mabao 11 ya Yanga msimu huu kati ya 28, waliyofunga timu nzima.
Ushindi huo wa Yanga unawafanya kufikisha pointi 42, katika michezo 16 na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi.
Kagera wao baada ya kupoteza wamekwenda nafasi ya nane katika msimamo wakiwa na pointi zao 20.
Kocha wa Kagera Sugar, Francis Baraza amesema baada ya kufungwa bao na Mayele wachezaji wake walipunguza hali ya kujiamini na kucheza tofauti na alivyokuwa anahitaji.
“Kuna shida kama kocha nimeziona katika mchezo huu tunakwenda kuzifanyia kazi ili kubadilika katika michezo inayofuata,” amesema Baraza na kuongeza;
“Tangu mechi na Biashara tulikuwa na mwenendo mzuri lakini Yanga wamekuja kuharibu rekodi hiyo ila siyo tatizo kubwa naenda kuwapushi wachezaji naimani tutarudi katika hali yetu.”
Kocha wa Yanga, Mohamed Nabi amesema wapinzani wao walikuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchezaji tofauti na ilivyokuwa mechi ya mzunguko wa kwanza kule Kaitaba Bukoba.
“Niwapongeze Kagera pamoja na kocha wao Baraza walikuwa bora ndio maana katika dakika 15, za mwanzo ni kama waliishika mechi,” amesema Nabi na kuongeza;
“Niwapongeze wachezaji wangu kwa kazi kubwa na walirudi mchezoni na kufanya vile ambavyo niliwaelekeza mpaka kupata mabao yaliyotupa ushindi mwingine leo.”