Yacouba atua Tunisia kuanza matibabu leo

Mshambuliaji wa Yanga Yacouba Sogne ametua salama nchini Tunisia tayari kwa matibabu ya goti lake la mguu wa kulia.

Daktari wa Yanga Youssef Mohamed amesema katika ratiba yao ya awali leo wataonana na Profesa ambaye atasimamia matibabu ya Yacouba.

Youssef amesema ratiba hiyo itaanzia katika vipimo vingine vitakavyofanywa na daktari Dahmane Jeleleddine ambaye ni daktari maalum kwa matibabu ya magoti pekee.

"Tumefika salama hapa Tunisia na tumeshafanya mawasiliano na Dokta Jeleleddine ambaye alikuwa anajua kwamba tutakuja hapa kufuatia mawasiliano yetu ya awali tukiwa Tanzania," amesema Yossef.

"Hatua hii ya sisi kufika hapa tu na kupata nafasi ya kuingia katika mpango wa matibabu ya daktari huyu kwanza niupongeze uongozi wa Yanga na GSM ambao gharama hizi ni kubwa,"

"Leo atafanyiwa vipimo upya ukiacha vile ambavyo vilibaini tatizo na baada ya hapo sasa majibu ya vipimo ndip yatatoa aina gani ya matibau ambayo Dokta Jeleledine ataona yanahitajika kufanyika."

Yacouba alipata tatizo la goti wakati akiitumikia Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting akilazimika kutolewa dakika ya 31 kipindi cha kwanza ambapo Yanga wamelazimika kumpeleka nchini Tunisia kwa matibabu kamili..