Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wydad yashinda mechi ya Ligi, ijayo vs Simba

Wapinzani wa Simba Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), timu ya  Wydad Casablanca leo Desemba 6 imecheza mechi ya Ligi Kuu Morocco na kushinda mabao 3-1 ikiifunga Mouloudia Club of Oujda.

Wydad itacheza dhidi ya Simba Desemba 9 jijini Marrakech katika mechi ya tatu hatua ya makundi CAFCL na kwa matokeo waliyopata leo yataamsha morali ikiwa ni timu pekee katika kundi B ambayo haina pointi hadi sasa wakifungwa mechi mbili za awali.

Simba ilicheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Novemba 9 dhidi ya Namungo na kutoka sare ya bao 1-1 na baada ya hapo imecheza mechi mbili za CAFCL dhidi ya ASEC Mimosas na Jwaneng Galaxy.