Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watatu waiangusha Twiga Stars Wafcon

TWIGA Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Bakari Shime, kuwakosa Aisha Masaka, Clara Luvanga na Opa Clement, limekuwa pigo kubwa na kusababisha kupoteza mchezo huo.

KICHAPO cha bao 1-0 ilichopokea Twiga Stars kwenye mchezo wa kwanza wa mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika Wanawake (WAFCON) inayoendelea nchini Morocco, imechangiwa na kukosekana kwa nyota watatu wa eneo la ushambuliaji.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Bakari Shime, kuwakosa Aisha Masaka, Clara Luvanga na Opa Clement, limekuwa pigo kubwa na kusababisha kupoteza mchezo huo.

Twiga Stars imepoteza mbele ya Mali katika mchezo huo wa kwanza wa Kundi C uliochezwa Julai 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Berkane, huku mfungaji wa bao hilo pekee akiwa kiungo mshambuliaji, Saratou Traoré dakika ya 45+1.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Shime alisema: “Tumewakosa wachezaji muhimu sana na bahati mbaya wawili tumewakosa hapa kwenye mashindano, Aisha aliumia wakati tupo kwenye maandalizi, hivyo tulimtoa kwenye mipango yetu.

“Lakini Clara aliumia juzi na Opah Clement kwa bahati mbaya amehama na kadi tatu alizozipata kwenye michuano ya mwanzo, nafikiri CAF wana kitu cha kuangalia kwa sababu wachezaji waliopambana miaka miwili nyuma wanahama na kadi, hii ibadilishwe.

“Kimsingi imeshusha morali ya wachezaji lakini kikosi changu kina chipukizi wengi wanaopata nafasi, ukiangalia kipindi cha kwanza walitetereka kutokana na ugeni wa mashindano lakini kipindi cha pili walijua nini cha kufanya.

“Mechi ilikuwa nzuri, tulimiliki kipindi cha kwanza tukitengeneza nafasi za kufunga lakini kwa bahati mbaya hatukuwa vizuri eneo la mwisho la kiwanja. Kipindi cha pili tulikuwa bora zaidi. Shida yetu kubwa ipo kwenye eneo la mwisho la kiwanja ambapo kwa bahati mbaya tuliwakosa wachezaji muhimu kama Aisha Masaka na Opah Clement hawakuwepo sehemu ya mchezo, mechi mbili zilizobakia tunaweza kurekebisha tulipokosea.”

Baada ya mchezo huo, Julai 11 Twiga Stars itakabiliana na Afrika Kusini ambayo imetoka kuichapa Ghana mabao 2-0 na kuongoza Kundi C. Kisha Julai 14, Twiga Stars itahitimisha hatua ya makundi kwa kukabiliana na Ghana.

Michuano hiyo iliyoanza Julai 5 inatarajiwa kufikia tamati Julai 26, 2025 ambapo Twiga Stars inashiriki kwa mara ya pili baada ya mwaka 2010 kuishia hatua ya makundi.