Wanariadha wa Kenya wang'ara mashindano FEASSSA

Muktasari:

  • Kenya imefanya vizuri kwenye mchezo wa riadha katika mashindano ya shule za msingi na sekondari kwa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki (FEASSSA) yanayoendelea jijini Arusha.

Wanariadha kutoka nchini Kenya wamefanikiwa kufanya vema katika Mashindano ya shule za msingi na sekondari Kwa nchi za Afrika mashariki (FEASSSA)  kunyakua jumla ya medali 37.

Mashindano hayo ya michezo mbali mbali yanayoendelea mkoani Arusha, Kwa Upande wa mchezo wa riadha wamefanikiwa kutamatisha Leo (Jana) September 21, huku Kenya wakivuna medali 37 wakifuatiwa na Uganda waliovuna medali 35 huku Tanzania wakivuna medali 18 na Rwanda wakipata Moja pekee.

Kenya ambao wametwaa ushindi wa Jumla Kwa Alama 366, walifanikiwa kuvuna medali 18 za gold, 10 za fedha na tisa za Shaba, huku Uganda wakivuna Alama 341, Kwa kupata medali 11 za Gold, 14 za fedha na Shaba 10.

Kwa Upande wa Tanzania walivuna Alama 240 zilizotokana na medali ya gold Moja, fedha sita na Shaba 11, huku Rwanda wakipata Alama 57 Kwa kuvuna medali Moja pekee ya Shaba.

Katika Mashindano hayo wanariadha hao walichuana katika vipengele  tofauti tofauti ikiwemo 100, 200, 1500, 5000, 10,000, kuruka juu na chini, miruko mitatu, mitupo, mikuki na tufe ambayo yote yamefanyika katika viwanja vya sheikh amri abeid Arusha.