Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wameipigia bao Chelsea wakiwa makinda Ligi ya Mabingwa Ulaya

Muktasari:

James bado hajajihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lakini bao lake hilo limemweka kwenye rekodi tamu kabisa katika kikosi cha Chelsea. Hii hapa ndio orodha ya wachezaji wenye umri mdogo kuwahi kuifungia Chelsea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya

LONDON, ENGLAND . REECE James amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuifungia bao Chelsea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati alipoweka wavuni kuisawazishia The Blues kwenye sare ya 4-4 dhidi ya Ajax uwanjani Stamford Bridge.

Akiwa na umri wa miaka 19, James ni moja ya makinda matata kabisa wanaotamba kwenye kikosi hicho cha Frank Lampard sambamba na Fikayo Tomori, Mason Mount, Callum Hudson-Odoi na kinara wao wa mabao, Tammy Abraham.

James bado hajajihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lakini bao lake hilo limemweka kwenye rekodi tamu kabisa katika kikosi cha Chelsea. Hii hapa ndio orodha ya wachezaji wenye umri mdogo kuwahi kuifungia Chelsea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Joe Cole (miaka 23, siku 150)?

Kiungo alitumikia maisha ya Stamford Bridge kwa miaka saba na hapo alifunga mabao 40 na kuasisti mara 42. Moja ya nyakati zake bora kabisa kwenye kikosi cha Chelsea ni kwenye ile mechi dhidi ya Bayern Munich ambapo alifunga bao kwenye ushindi wa 4-2 kuisaidia The Blues kuwachapa` miamba hiyo ya Bundesliga kwa jumla ya mabao 6-5 na kutinga hatua ya nusu fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2005.

Tammy Abraham (miaka 22, siku 0)

Katika siku yake ya kuzaliwa, straika wa Chelsea, anayetamba kwa sasa, Tammy Abraham aliweka rekodi ya kufunga bao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati alipofunga la kuongoza kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Lille msimu huu. Hiyo ilikuwa kuirudisha Chelsea kwenye moto wake baada ya kupoteza katika mchezo uliotangulia, dhidi ya Valencia. Tammy alipigiwa asisti na kinda mwenzake, Fikayo Tomori. Kocha, Frank Lampard amewekeza imani kubwa sana kwa wachezaji vijana.

Kurt Zouma (miaka 21, siku 28)

Kurt Zouma aliibukia kwenye kikosi cha Chelsea mwaka 2014, kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenye timu kadhaa kwenda kunoa zaidi akili yake ya mpira. Sasa amerudi tena Stamford Bridge na panga pangua yupo kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Frank Lampard. Lakini, akiwa bado mdogo, Zouma aliweka rekodi ya kuwa mmoja wa wachezaji wenye umri mdogo kuifungia Chelsea bao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, alipofanya hivyo dhidi ya Maccabi Tel Aviv mwaka 2015. Chelsea ilishinda 4-0.

Daniel Sturridge (miaka 21, siku 14)

Kuna watu watakuwa wamesahau kwamba Daniel Sturridge aliwahi kuichezea Chelsea. Lakini, alifanya hivyo na mwaka 2010 aliweka rekodi ya kufunga bao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na umri mdogo, kipindi hicho alipofunga bao la kusawazisha dhidi ya MSK Zilina, kabla ya Florent Malouda kuja kufunga la ushindi. Maisha yake ya Stamford Bridge, Sturridge hayakuwa matamu sana kwa kulinganisha na yale aliyokwenda kuishi huko Anfield, alipokuwa akiitumikia Liverpool.

Oscar (miaka 21, siku 10)

Muda mfupi baada ya kutimiza umri wa miaka 21, kiungo Kibrazili, Oscar alifunga si mara moja, bali mbili dhidi ya Juventus katika kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2012.

Hakika bao lake la pili litabaki kwenye kumbukumbu za kudumu za mashabiki wa Chelsea kutokana na kile alichowafanyia Leonardo Bonucci na Andrea Pirlo kabla ya kufunga bao hilo. Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 2-2, huku Oscar akiondoka nyumbani na rekodi yake.

Arjen Robben (miaka 20, siku 284)

Mdachi Arjen Robben sasa anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa pili mwenye umri mdogo kuifungia Chelsea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati alipofanya hivyo kwenye mechi ya makundi dhidi ya CSKA Moscow.

Chelsea wakati huo ikiwa chini ya Kocha Jose Mourinho, ilikuwa kwa mara ya kwanza kwa kocha huyo kuwaanzisha kwa pamoja Robben na Damien Duff na hakika mambo yalikuwa matamu uwanjani.

Reece James (miaka 19, siku 332)

Baada ya kucheza kwa mkopo Wigan msimu uliopita, msimu huu unaonekana kuwa mtamu zaidi kwa kinda huyo wa Chelsea, Reece James.

Kiwango chake kwenye mchezo dhidi ya Ajax kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ulikuwa moto kwelikweli hasa ukizingatia timu yake ya Chelsea ilikuwa nyuma kwa mabao 4-1.

Baada ya Chelsea na matokeo kuwa 4-3, James alihitaji kuweka historia ya kuisawazishia The Blues katika mchezo huo uliopigwa Stamford Bridge na Ajax walicheza wakiwa pungufu.