Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Walles Karia achukua Jembe Mwanaspoti

MWANDISHI Mwandamizi wa Mwanaspoti, Gift Macha ameteuliwa na Rais wa Shirikisho la soka Tanzania Walles Karia kuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya tuzo mbalimbali za Ligi Kuu Bara inayoendelea.

Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema rais ameyapitisha majina hayo ili kuwa na  kamati ambayo itakuwa inasimamia  tuzo zote ambazo zitakuwa zinatolewa katika ligi.

Mwenyekiti wa kamati  hiyo atakuwa Ahmed Mgoyi, Makamu Mwenyekiti ni Almasi Kasongo, Katibu Mkuu ni Amiri Mhando.

Na wajumbe wa kamati hiyo watakuwa wanane ambao nao wametoka katika vyombo mbalimbali vya habari hususan vinavyohusika moja kwa moja na musuala ya michezo hapa nchini.

Wajumbe wengine waliochaguliwa na Karia ni pamoja na Patrick Kahemele, Saleh Ally, Kenny Mwaisabula, Ibrahim Masoud ‘Maestro’, Fatma Likwata, Said George na Zena Chande.