Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wahabeshi waitangulia Yanga CAF

Muktasari:

  • CBE ilikuwa ikirudiana na SC Villa ya Uganda katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Abebe Bikila, jijini Addis Ababa na mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1 na kuwafanya wenyeji kufuzu raundi ijayo kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.

WAKATI Yanga ikijiandaa kushuka uwanjani saa 1:00 usiku kumalizana na Vital'O ya Burundi, wapinzani watakaokutana nao katika raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kama itawang'oa Warundi, CBE ya Ethiopia yenyewe imetangulia mapema baada ya muda mchache uliopita kulazimishwa sare nyumbani.

CBE ilikuwa ikirudiana na SC Villa ya Uganda katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Abebe Bikila, jijini Addis Ababa na mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1 na kuwafanya wenyeji kufuzu raundi ijayo kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.

CBE ilishinda mechi ya kwanza ugenini kwa mabao 2-1 na sasa imejikwa tayari ikiisubiria Yanga inayorudiana na Vital'O ambayo ilipoteza katika mechi ya kwanza wiki iliyopita kwa mabao 4-0 na hivyo kuhitaji kuichapa Vijana wa Jangwani mabao yasiyopungua 5-0.

Mbali na CBE, timu nyingine zilizotinga raundi ya pili ni Black Bulls ya Msumbiji na Stellenbosch ya Afrika Kusini zilizojihakikishia nafasi hizo kupitia michuano ya Kombe la Shirikisho.