Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadada atajwa Singida BS

Muktasari:

  • Habari ambazo Mwanaspoti linazo ni kwamba Wadada tayari ameshamalizana na mabosi wa Singida na kilichobaki anasubili dirisha la usajili lifunguliwe na atangazwe.

KLABU ya Singida Big Stars imeendelea kujiimarisha kwenye eneo lake la ulinzi baada ya kudaiwa  kukamilisha usajili wa beki wa kulia Nicolas Wadada anayecheza katika kikosi cha Ihefu.
Huu ni usajili wa pili kwa Singida Big Stars baada ya kukamilisha usajili wa Yahya Mbegu ambaye waliipokonya Simba tonge mdomoni.

Habari ambazo Mwanaspoti linazo ni kwamba Wadada tayari ameshamalizana na mabosi wa Singida na kilichobaki anasubili dirisha la usajili lifunguliwe na atangazwe.

Inadaiwa mabosi wa Singida wanataka eneo la beki ya kulia kuwe na watu wenye uzoefu kwani tayari ilishamtoa kwa mkopo Juma Abdul kwenda Kitayosce hivyo kwa sasa imebaki na beki wa asili Paul Godfrey ambaye na yeye hapati nafasi ya kucheza mbele ya Nicolas Gyan.

Gyan amelazimika kucheza eneo hilo licha ya kwamba yeye anamudu vyema kucheza kama kiungo mshambuliaji (Winga) au mshambuliaji wa kati, lakini akiwa kama beki wa kulia bado ameonyesha kiwango kizuri.

Mabosi wa Singida wamelazimika kukamilisha usajili wa Wadada kwa ajili ya kumpa sapoti Gyan kwani pindi anapokuwa ameumia basi eneo hilo limekuwa likilega lega.
Kuingia kwa Wadada kutatoa mwanga kwa benchi la ufundi la Singida kwani eneo hilo tayari kutakuwa na wachezaji wawili ambao wana kiwango kizuri na kikubwa wakiwa wanaenda kimataifa.

Wadada upande wa Ihefu ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo kikosi cha kwanza kwenye timu hiyo msimu huu hivyo kuondoka kwake ni Singida BS kuchomoa mchezaji wa pili tegemeo kwenye timu hiyo baada ya kufanya kwa Mbegu.
Wadada alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Ihefu ambao unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Afisa habari wa Singida Bs Hussein Masanza alipoulizwa juu ya usajili wa Wadada alisema kwa kifupi; "Tusubiri hadi Ligi imalizike kila kitu kitakuwa wazi, kwa sasa Wadada ni mchezaji wa Ihefu kwa hiyo siwezi kuzungumzia sana.".