Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachezaji hawa watauana kusaka namba yaibuka Ligi Kuu

Muktasari:

Utitiri wa wachezaji waliosajiliwa wanaocheza nafasi ya ushambuliaji unaashiria eneo hilo ndilo litakuwa na ushindani mkali kwa timu mbalimbali wakati huu wa maandalizi.

Dar es Salaam. Wakati kambi za maandalizi ya msimu mpya zikipamba moto kwa timu mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara, ushindani wa namba kwa wachezaji ni moja ya mambo yanayonogesha maandalizi hayo.
Usajili uliofanywa na klabu zinazoshiriki Ligi Kuu, ni wazi umeibua vita ya namba katika kipindi hiki ambayo inahusisha wachezaji wa nafasi mbalimbali wanaopigania kuwemo katika kikosi cha kwanza msimu ujao ndani ya timu hizo.
Ikumbukwe ndani ya kipindi hiki cha maandalizi, ndipo makocha hupata taswira ya vikosi vya kwanza vya timu zao vitakavyokuwa msimu unaofuata.
Utitiri wa wachezaji waliosajiliwa wanaocheza nafasi ya ushambuliaji unaashiria eneo hilo ndilo litakuwa na ushindani mkali kwa timu mbalimbali wakati huu wa maandalizi.
Tathmini iliyofanywa na gazeti hili kwa kutazama vikosi vya timu nne zitakazoshiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao ambazo ni KMC, Yanga, Azam na Simba imebaini kuwa nyota wa timu hizo kila mmoja anapaswa kutumia vyema kipindi hiki kujitafutia nafasi katika kikosi cha kwanza.
Mfano ndani ya Simba, washambuliaji wanaowania nafasi kikosini ni Meddie Kagere, Wilker Da Silva, Deo Kanda, Miraji Athumani, John Bocco, Rashid Juma na Ibrahim Ajibu.
Kwa Yanga kuna Juma Balinya, Maybin Kalengo, Sadney Urikhob, Mrisho Ngassa, Patrick Sibomana na Issah Bigirimana.
Ndani ya Azam wamo Idd Selemani ‘Nado’, Obrey Chirwa, Donald Ngoma, Kassim Khamis, Idd Kipagwile, Selemani Ndikumana, Emmanuel Mvuyekure, Richard Djodi na Joseph Mahundi ambao wanaocheza nafasi ya ushambuliaji.
Nao KMC itakuwa na vita itakayowahusisha Hassan Kabunda, Cliff Buyoya, James Msuva, Ramadhani Kapera, Salim Aiyee, Vitalis Mayanga na Charles Ilanfya.
Kwa upande wa kiungo, Simba itakuwa na vita baina ya Clatous Chama, Francis Kahata, Hassan Dilunga, Sharaf Shiboub, Said Ndemla na Mzamiru Yassin wakati kwa Yanga kuna ushindani baina ya Said Juma, Papy Tshishimbi, Feisal Salum, Gustav Saimon, Abdulaziz Makame, Mohammed Issah na Mapinduzi Balama.
Vita ya viungo kwa Azam itakuwa baina ya Salum Abubakar, Frank Domayo, Mudathir Yahaya wakati kwa KMC itawahusisha Reyman Mgungila, Ismail Gambo, Kenny Ally na Ally Msengi.
Mabeki Mohammed Hussein, Shomari Kapombe, Tairone Santos, Gerson Vieira, Paschal Wawa, Erasto Nyoni, Yusuph Mlipili na Gadiel Michael watakuwa wakipigania nafasi ya kuanza kikosi cha Simba kama ilivyo kwa Selemani Mustafa, Lamine Moro, Jafari Mohammed, Juma Abdul, Kelvin Yondani na Paulo Godfrey kwa Yanga.
Azam itakuwa na ushindani baina ya mabeki Yakub Mohammed, Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, David Mwantika na Oscar Masai na upande wa KMC ni akina Sadallah Lipangile, Ally Oviedo, Abdallah Mfuko na wengineo.
Mbali na vita hiyo ya namba, makocha wa timu hizo watakuwa na kibarua kigumu cha kutengeneza muunganiko mzuri wa timu hasa baada ya timu hizo kuondokewa na nyota waliokuwa tegemeo kwenye kikosi cha kwanza.
Azam imeondokewa na viungo Stephan Kingue na Tafadzwa Kutinyu na winga Enock Atta wakati KMC imeondokewa na beki Ally Ally.
Upande wa Simba itakuwa bila James Kotei, Haruna Niyonzima, Zana Coulibaly, Juuko Murushid na Emmanuel Okwi wakati Yanga haitokuwa na Makambo Heritier, Gadiel Michael na Ibrahim Ajibu katika  mashindano ya msimu ujao.