Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wabongo, Wakenya wakabana magari

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa waandaji kutoka Klabu ya Mount Usambara, kuna mchakato wa kuwaleta Tanga madereva bingwa kutoka Mombasa nchini Kenya na kwa mujibu wa mwenyekiti wa klabu hiyo, Hussein Moor, ujio wa madereva hao utathibitishwa  mapema juma hili.

ITAKUWA ni mchuano mkali kati ya madereva wa Tanzania na Kenya katika mwezi huu wakati harakati za kuwaleta nchini washiriki kutoka Mombasa zikifikia hatua ya kuridhisha.

Kwa mujibu wa waandaji kutoka Klabu ya Mount Usambara, kuna mchakato wa kuwaleta Tanga madereva bingwa kutoka Mombasa nchini Kenya na kwa mujibu wa mwenyekiti wa klabu hiyo, Hussein Moor, ujio wa madereva hao utathibitishwa  mapema juma hili.

“Tuko katika hatua za mwisho za kukamilisha mchakato wa kuwadhamini madereva watatu, na majina yao na aina za magari watakayoyatumia vitawekwa bayana mapema juma hili,” alisema Moor na kusisitiza kuwa tarehe ya mashindano ni Julai 20 na 21 mwaka huu.

Akiendelea, Moor alisema umbali wa njia kuu ya mashindano ni kilomita 155  na madereva na magari yao watachuana katika maeneo yenye vivutio vya utalii vya maeneo ya Pongwe, Mkanyageni na Mlamleni.

Miongoni mwa madereva waongozaji (naviagtors) watakaozinogesha mbio za magari mwaka huu ni Mzambia David Sihoka ambaye ni mmoja wa magwiji wa  daraja la juu barani Afrika.

Sihoka, ambaye amekuwa akimuongoza dereva Muna Singh wa Zambia kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, safari hii atakuwa na dereva kutoka Arusha, Gurpal Sandhu wakiendesha gari aina ya Mitsubishi Evo 10, akiwa ni mzoefu sana wa barabara za Tanzania.

Kwa mujibu wa Moor, Kuwepo kwa madereva vinara wa mbio za magari kutazidisha ushindani.