Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waamuzi wa Simba, Yanga kimataifa hawa hapa...

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf), limempanga refa Patrice Tanguy Mebiame (30) kutoka Gabon kuchezesha mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Merrikh ya Sudan utakaochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Septemba 30 kuanzia saa 1:00 usiku huku Simba itakayocheza na Power Dynamos uwanjani hapo Oktoba Mosi, ikipewa refa wa Libya, Mutaz Ibrahim.

Mwamuzi Mebiame atakayechezesha mechi ya Yanga amekuwa na neema kwa timu za nyumbani ambazo zimekuwa na historia ya kupata ushindi pindi anaposhika filimbi huku akigeuka shubiri kwa zile ambazo zinakuwa ziko ugenini.

Kumbukumbu inaonyesha kuwa refa huyo aliyepata beji ya uamuzi ya kimataifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa mara ya kwanza mwaka jana, amechezesha mechi sita za kimataifa ambazo zote zilimalizika kwa timu iliyokuwa nyumbani kupata ushindi.

Ni refa anayeonekana sio mnoko sana kwani katika mechi hizo sita alizochezesha, ameonyesha idadi ya kadi 20 tu ikiwa ni wastani wa kadi 3 kwa mchezo, ambapo kadi 19 ni za njano na moja ni nyekundu.

Katika mchezo huo wa Jumamosi ijayo, Yanga inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili iweze kutinga hatua ya makundi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Kigali, Rwanda.

Kwa upande wa Simba, mechi yao dhidi ya Power Dynamos itachezeshwa na refa Mutaz Ibrahim kutoka Libya ambaye ameonekana kutokuwa na uzoefu mkubwa na mechi za kimataifa.

Mwamuzi Ibrahim naye amekuwa na bahati na timu zinazokuwa nyumbani kwani katika mechi 10 zilizopita za mashindano ya Klabu Afrika ambazo amechezesha, timu zilizokuwa nyumbani ziliibuka na ushindi mara tano, sare mbili na wageni walishinda mara moja tu.

Katika mechi hizo, refa huyo ameonekana hana mzaha na wacheza rafu na wachezaji watovu wa nidhamu kwani ameonyesha idadi ya kadi 37, njano zikiwa ni 36 na nyekundu moja.

Mutaz mwenye umri wa miaka 33, kwa mara ya kwanza alipata beji ya uamuzi ya FIFA mwaka 2019.

Habari za uhakika ambazo mwanaspoti tumezipata ni kuwa refa Mutaz atasaidiwa na Salm Agha kutoka Libya, Ahmed Ibrahim kutoka Misri na Hassan Khalil kutoka Tunisia.

Simba baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 katika mechi ya kwanza ambayo ilikuwa ugenini huko Zambia, inahitaji ushindi wa aina yoyote katika mechi ya marudiano ili itinge hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Nyota wa zamani wa Yanga, Hery Morris alisema kuwa Simba na Yanga zinapaswa kujiandaa kushinda uwanjani pasipo kumtegemea mwamuzi.

“Rekodi ya mwamuzi hata wao bila shaka wameshaiona, kikubwa ni kuendelea kuwatengeneza kisaikolojia wachezaji.

“Kazi ukitaka iwe bora ni lazima uwe na nidhamu kwahiyo wachezaji inabidi wawe na nidhamu ya hali ya juu,” alisema Morris.