Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita 7 ndani ya Yanga

Donald Ngoma

Muktasari:

Wakati kazi hiyo ikiendelea tayari kuna vita vya chini chini kwa wachezaji katika kuwania nafasi imeanza kujitokeza ambapo wako wanaonyesha watapoteza nafasi zao kama ambavyo walivyojituma katika msimu uliopita, lakini pia wapo wapya ambao wanahitaji kuonyesha uwezo kuchukua nafasi katika kikosi cha makocha Hans Pluijm na Boniface Mkwasa.

YANGA inatafuta kikosi chake cha kwanza kwa sasa wakati huu inapokaribia michuano ya Kombe la Kagame, hatua hiyo inakuja kufuatia usajili ambao timu hiyo imeufanya katika dirisha hili la usajili.

Wakati kazi hiyo ikiendelea tayari kuna vita vya chini chini kwa wachezaji katika kuwania nafasi imeanza kujitokeza ambapo wako wanaonyesha watapoteza nafasi zao kama ambavyo walivyojituma katika msimu uliopita, lakini pia wapo wapya ambao wanahitaji kuonyesha uwezo kuchukua nafasi katika kikosi cha makocha Hans Pluijm na Boniface Mkwasa.

Chini ni orodha ya vita saba vinavyopiganwa chini kwa chini baina ya wachezaji katika kusaka heshima mbele ya makocha wao kabla ya kuanza kwa Kombe la Kagame na msimu mpya wa ligi.

Mwinyi/Joshua

Wote hawa wanacheza beki ya kushoto, katika mchezo uliopita kati ya Yanga na KMKM ulikuwa ni jibu tosha kuna ingizo jipya Mwinyi Haji Mngwali ambaye ataingia vitani kugombea namba na Oscar Joshua ‘OJ’, lakini tayari Mwinyi ameanza kuonyesha mambo tofauti na Joshua.

Beki huyu aliyesajiliwa kutoka KMKM anaonekana kuwa imara kwa kupandisha mashambulizi na hata kushambulia kwa kupiga mashuti makali yenye maana kitu ambacho Joshua anapungukiwa kidogo hasa katika maamuzi ya mwisho juu ya afanye nini anapokuwa anapanda mbele.

Wakati ubora wa Mwinyi ukiwa hivyo Joshua naye ana ubora wake katika ukabaji hataki masihara Mwinyi kidogo anatakiwa kujifunza katika hili kwa mkongwe huyu, ingawa wengi tayari wanaona kuwa, nafasi ya Joshua katika kikosi cha kwanza kwa sasa mbele ya dogo hili la Kizenji ni ndogo.

Zuttah/Abdul

Mabeki wa kulia hawa Juma Abdul alikuwepo katika msimu uliopita na akafanya kazi kubwa kiasi cha wadau kupendekeza kwamba alistahili kuwepo katika kikosi cha Taifa Stars, lakini Yanga ikaona haitoshi ikamleta Mghana Joseph Zuttah katika nafasi hiyo.

Hakuna mtu ndani ya Yanga atasahau ubora wa Abdul katika msimu uliopita alifanya kazi safi ya kukaba na kupandisha mashambulizi, lakini kuna muda anapungukiwa na ubora zaidi katika kurudi kukaba wakati amepanda kushambulia anahitaji kupambana na Zuttah ambaye bado hajaonyesha kuwa imara zaidi.

Zuttah ni mzuri katika kupiga krosi lakini katika mchezo uliopita uliokuwa wa kwanza kwake ndani ya Yanga hakuwa imara katika kukaba, ingawa alionekana kwamba anaweza hata kucheza kama kiungo hasa juu ya maamuzi ake ya kupiga pasi za haraka na kuwapunguza wapinzani. Pia kuna muda kama anajisahau kidogo akichelewa kufanya maamuzi.

Ngoma/Tambwe

Wakali hawa wote ni washambuliaji wa kati, hakuna sababu ya kuelezea makali ya Amissi Tambwe, ukibisha subiri mabeki wazubae kumkaba uone anafanya nini anachojua yeye ni kufunga tu, lakini sasa ameletewa mtu mwingine Mzimbabwe Donald Ngoma.

Haitakuwa kazi rahisi kwa Ngoma kumfanya Tambwe apotee na kuna wasiwasi wanaweza kuwa chaguo la kwanza wote wakaanza katika kikosi kimoja ubora wao uko hivi.

Tambwe anaweza kuwa chaguo la Pluijm kwa kuwa amefanikiwa kuweza kufunga mabao mengi akifunga mabao 16 ndani ya kikosi hicho msimu uliopita 14 yakiwa ya Ligi Kuu na mengine ya Kombe la Shirikisho Afrika (bao la 17 alitoka nalo Msimbazi), huku pia akionyesha ubora katika kurudi kusaidia majukumu ya ukabaji.

Ngoma naye hayuko nyuma anajua kuficha mpira na kuwakimbiza haa mabeki watatu ameonyesha makali hayo juzi dhidi ya KMKM ni kama Didier Kavumbagu mpya katika kikosi hicho lakini pia anajua kufunga kutakuwa na vita hapa wataamua wenyewe makocha mimi simo.

Sherman/Busungu

Kpah Sherman ni kama amezaliwa upya, ameonyesha safari hii amekuja kupigania namba yake na heshima ndani ya kikosi hicho, anajiamini anatoa mpira kwa haraka kwa kujua kuwachezesha wenzake bado kidogo suala la kulenga lango ni shida aliyobaki nayo, atakuwa na vita na Malimi Busungu ingizo jipya hili.

Busungu hadharauliki kutokana na kuja na ubora wake wa kuwa mviziaji mzuri mwenye shabaha ukizubaa kidogo kumkaba anakufunga sio tu kwa miguu yake, hata kichwa chake lakini pia sio mchoyo anaweza kuwachezesha wenzake kazi itakuwepo.

Telela/Niyonzima

Hawa wote walikuwepo msimu uliopita ni vigumu kumshusha thamani Haruna Niyonzima kwa ajili ya Salum Telela, lakini endapo Mnyarwanda huyu asipoamka anaweza kujikuta akikasimu madaraka kwa Telela.

Achana na uwezo wa kawaida aliouonyesha Telela dhidi ya KMKM ni kutokana na kuwa katika mfungo wa Ramadhani, lakini endapo akipewa majukumu ya kufanya kazi katika nafasi ya kiungo wa juu au hata chini anaweza kukufanyia waulize Etoile du Sahel kilichowapata yule Frank Kom aliyesumbua Uwanja wa Taifa kule alijikuta akicheza rafu na kutolewa kwa kadi nyikundu.

Kaseke/Msuva

Ukichunguza ni kama Simon Msuva thamani yake ndani ya Yanga imeshuka vile, lakini mimi nasema bado ana nafasi kubwa licha ya kwamba kuna mtu anaitwa Deus Kaseke ameingia na kila mmoja ana ubora wake.

Msuva anajua kufunga hili lipo wazi, lakini pia kasi yake hakuna mchezaji ndani ya nchi hii amejaliwa ni vigumu kumshusha thamani yake, ingawa anatakiwa kubadilika katika maamuzi yake ya mwisho akiwa kiungo wa pembeni kwa kuwa na hali ya kuwafikiria kwanza washambuliaji wa kati.

Kaseke naye ana vitu vyake ana nguvu sio rahisi kumuangusha, lakini pia anajua kuchezesha timu huu ni ubora achana na hilo pia anaweza kucheza kama kiungo wa kati usajili mzuri.

Twite/Makapu

Kwa sasa hakuna namna Yanga inamchezesha mkongwe Mbuyu Twite kama kiungo mkabaji anaweza kucheza hapo, lakini sio kwa ubora mkubwa kutokana na bado mzito kumudu hapo lakini atafanya kazi hapo kutokana na Said Makapu hayupo.

Kijana huyu ana ubora wake ni mwepesi kukaba kwa nguvu, lakini tatizo lake ni pasi za haraka amepungukiwa jambo ambalo Twite ni rahisi huwezi kumpokonya ubora wake katika kupiga pasi safi zinazofika. Kwa hali hiyo ni wazi hivi si vita vya kitotot yeyote atakayezubaa imekula kwake.