Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana yaduwazwa na Ukonga Kings nusu fainali RBA

Muktasari:

Ukonga Kings iliyoongozwa na Junior Kabeya aliyefunga pointi 13 na Fredrick Seba aliyefunga pointi 11 ilionyesha utulivu zaidi kota ya tatu licha ya kuzomewa na mashabiki wa Vijana.

Dar es Salaam.Vigogo wa mpira wa kikapu, timu ya vijana imeanza kwa kipigo mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya mkoa wa Dar es Salaam (RBA) inayoendelea.

Vijana iliduwazwa kwa kipigo cha pointi 69-52 kutoka kwa Ukonga Kings katika mchezo uliokuwa na ushindani mkali uliofanyika kwenye uwanja wa Bandari Kurasini, Dar es Salaam.

Ukonga Kings ilianza vizuri kota ya kwanza kujihakikishia ushindi kota ya tatu na nne baada ya kupoteza kota ya pili.

Ukonga Kings inayonolewa na kocha Denis Funganoti ilianza vizuri kota ya kwanza kwa kuongoza kwa pointi 22-12.

Licha ya Vijana kujitutumua na kuongoza kota ya pili kwa pointi 13-05 na kuifanya kwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa tofauti ya pointi mbili ya matokeo ya 27-25, lakini hawakuweza kuendeleza kasi hiyo kwenye kota ya tatu ambako walitumia mbinu ya kufunga kwa 'three point' lakini mipira yao mingi ya mwisho iliishia kugonga nje ya goli na kuokolewa na wachezaji wa Ukonga Kings ambao hawakuwapa Vijana mwanya wa kufunga kirahisi.

Hadi kota hiyo inamalizika, Vijana ilikubali kipigo cha pointi 30-21 huku kota ya mwisho na ya lala salama nyota wa vijana wakidhibitiwa na kuruhusu kipigo cha pointi 12-05  ambapo hadi filimbi ya mwisho Ukonga Kings ilitoka  kifua mbele kwa ushindi wa pointi 69-52.

Licha ya nyota wa vijana, Jonas Mushi kuongoza kwa kufunga pointi nyingi katika mchezo huo akifunga pointi 13 akifuatiwa na Anthony Jeikanga aliyefunga pointi 12 lakini hawakuweza kuisaidia timu yao kuondoka na ushindi.

Ukonga Kings iliyoongozwa na  Junior Kabeya aliyefunga pointi 13 na Fredrick Seba aliyefunga pointi 11 ilionyesha utulivu zaidi kota ya tatu licha ya kuzomewa na mashabiki wa Vijana, ilitulia na kucheza kwa kuelewana huku baadhi ya wachezaji wa Vijana mara kwa mara katika kota ya tatu walionekana kuwalalamikia waamuzi.

Katika mechi hiyo, Junior Kabeya tena wa Ukonga Kings alikuwa mchezaji aliyeongoza kwa kufunga pointi tatu 'three point' akifunga mara 4 wakati Joseph Mshana wa vijana akiongoza kwa kuokoa mipira ya mwisho 'rebound' ambazo aliokoa mara 11 na Oscar Azan wa Ukonga Kings aliongoza kutoa pasi za mwisho 'Assist' ambazo alitoa mara tano.

Kwa matokeo hayo, Vijana sasa inahitaji ushindi katika michezo miwili (game two na three) ili kujihakikishia kufuzu kucheza fainali.

Endapo atafungwa kwenye 'game two' Ijumaa ijayo basi safari ya Vijana kwenye RBA itakuwa imeishia hapo huku akimpa nafasi Ukonga Kings ya kutinga fainali ambayo atacheza na mshindi wa mechi kati ya  Savio na Kurasini Heat itakayochezwa leo Alhamisi.