Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Makambo, Ngassa wauwasha moto Yanga

Muktasari:

Kutokana na matokeo hayo Yanga imepanda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi 29, wakiwapita  watani wao Simba wanaocheza leo Ijumaa na Lipuli FC wao wako nafasi ya tatu na pointi 26. Vinara ni Azam FC wenye 33.

YANGA jana iliendeleza rekodi yao ya kutopoteza mechi katika Ligi Kuu msimu huu baada ya kuifumua Mwadui FC mabao 2-1, lakini gumzo kwenye mchezo huo akiwa kipa Nkizi Kindoki aliyewachefua mashabiki wa Yanga wa mjini hapa.
Kipa huyo aliyesajiliwa msimu huu akitokea klabu ya Racing da Kinshasa ya kwao DR Congo ili kuchukua nafasi ya Youthe Rostand, aliwatibua mashabiki baada ya kuruhusu bao la kusawazisha dakika chache kabla ya mapumziko.
Yanga ikiwa mbele kwa bao la mapema la dakika 10 kutoka kwa Heritier Makambo, kwenye mchezo huo wa kiporo uliopigwa Uwanja wa Kambarage, kipa huyo alishindwa kudaka mpira wa krosi uliopigwa na Charles Ilanfya baada ya kumgonga kifuani na kumpa nafasi Salum Aiyee kufunga bao kiulaini.
Bao hilo alilofungwa Kindoki ni la nne kwa kipa huyo katika mechi nne alizodaka lilimtibua mpaka kocha wake, Mwinyi Zahera ambaye alionekana kumfokea kabla ya kufanya kumtoa kipindi cha pili na kumuingiza Ramadhani Kabwili.
Mashabiki wa Yanga wa Shinyanga nao hawakumuacha salama, walimzomea na kumtaka atolewe jambo lililomfanya kipa huyo kumwaga chozi akiwa kwenye benchi la Yanga kuonekana wazi akijutia kilichomkuta.

NGASSA ATOA ZAWADI
Achana na bao la Makambo, mkongwe Mrisho Ngassa aliendelea kuthibitisha kuwa bao wamo na Yanga haikufanya makosa kumrejesha Jangwani baada ya kuupiga mpira mwingi, huku akiifunga timu yake bao la ushindi.
Bao hilo limemfanya Ngassa kufikisha mabao matatu na mara baada ya mchezo huo alisema amelitoa kama zawadi kwa mwanawe aliyetimiza mwaka mmoja tangu azaliwe ambaye jana ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.
Ngassa alifunga bao hilo dakika ya 58 kwa shuti akimalizia pasi ya Maka Edward
na shuti hilo kumshinda kipa wa Mwadui, Mussa Mbissa na kuifanya Yanga ifikishe alama 29 baada ya kucheza mechi 11 na kuchupa hadi nafasi ya pili.

MCHEZO ULIVYOKUWA
Yanga ililianza pambano hilo kwa kishindo licha ya kuwakosa nyiota wake kadhaa akiwamo Nahodha, Kelvin Yondani na Kipa Beno kakolanya waliosalia jijini Dar es Salaam na Ibrahim Ajibu aliyekuwa na kikosi mjini hapa lakini hakucheza.
Inaelezwa Ajibu hakuwa anahudhuria mazoezi na hivyo kuonekana kutokuwa fiti na alikuwa kivutia alipojichimbia kwenye gari na kufuatwa na mashabiki wa Yanga waliokuwa wakimshangilia mwanzo mwisho.
Baada ya kosa kosa kwa dakika za mapema, Mkongoman, Makambo aliwanyanyua mashabiki wa Yanga kwa kufunga bao baada ya kupokea pasi katika shambulizi alilolianzisha mwenyewe na kuwahadaa mabeki kwa kupiga shuti kali pembeni mwa lango la Mwadui. Hilo lilikuwa bao la tano kwa Makambo katika Ligi Kuu mpaka sasa.
Mwadui walicharuka kutaka kusawazisha lakini ukuta wa Yanga ulikuwa chini ya Andrew Vincent 'Dante' na Abdallah Shaibu 'Ninja' uliwanyima bao mpaka dakika ya 40 pale Kindoki alipofanya makosa yaliyompa nafasi Salum Aiyee kufunga bao, linalokuwa la pili kwake msimu huu.
Kindoki ndani ya dakika 45 alizocheza alionekana kufanya makosa mengi ambayo kama mastraika wa Mwadui wangekuwa makini wengeweza kufunga bao zaidi ya hilo moja  na pengine kuitibulia timu yake rekodi tamu iliyonayo mpaka sasa.
Yanga waliingia kipindi cha pili kwa kufanya mabadiliko kwa kumtoa Kindoki na nafasi yake kuingia Kabwili na Matheo Anthony akichukua nafasi ya Gadiel Michael kabla ya Rafael Daud kumpokea Amissi Tambwe dakika ya 61.
Mabadiliko ya Michael yalimfanya Jaffary Mohammed kurudi nyuma kuziba nafasi ya beki huyo wa kushoto na nafasi ya kiungo huyo mbele kuzibwa na Matheo.
Katika mchezo huo Yanga ilizidiwa umiliki wa mpira baada ya wenyeji kupata asilimia 56 dhidi ya 44 za Vijana wa Jangwani, huku ikipta kadi mbili za njano za Ninja na Jaffar dhidi ya tatu za Mwadui.
Yanga ilipata kona tano dhidi ya nne za Mwadui na walifanya faulo 17 dhidi ya 19 za wenyeji, huku wakipiga mashuti nane, manne yakilenga lango na mengine yakitoka nje.
Mwadui wao waliopiga mashuti 15, manne yakilenga lango na 11 yakitoka pembeni, huku Kocha Mkuu wa Yanga akisifu vijana wake akisisitiza anashukuru kwa ushindi ikiwa mechi yao ya kwanza ugenini.
"Tunachotaka ni ushindi bila kujali tunacheza na nani na kwenye uwanja gani, muhimu kufikia malengo yetu," alisema Zahera huku Kocha wa Mwadui akisema timu yake ilikosa bahati licha ya kutawala pambano hilo kwa muda mrefu.
Yanga inarudi jijini Mwanza kabla ya kuanza safari ya kuelekea Bukoba kuwahi pambano laop la Jumapili dhidi ya Kagera Sugar litakalopigwa Uwanja wa Kaitaba.