Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usajili Yanga waitesa Simba

Jengo la klabu ya Yanga

MWANDISHI WETU YANGA inaitegea Simba na hilo huenda likaitesa klabu hiyo ya Msimbazi kipindi chote cha usajili mdogo. Viongozi wa Yanga wamedai kuwa watafanya usajili wa dirisha dogo kimyakimya na inawezekana wakakamilisha kazi hiyo dakika za mwisho kabisa za usajili wa dirisha dogo. Wachezaji wanaotajwa kuwa huenda wakaingia Jangwani katika dirisha dogo ni beki wa kati wa Simba, Kelvin Yondani 'Vidic' jambo ambalo Msimbazi hawataki kusikia hata kidogo. Hata hivyo hakuna uhakika kama Mohammed Banka na Athuman Idd 'Chuji' wanaweza kusajiliwa katika timu hiyo ya Kosta Papic. Simba imepata hofu zaidi na hata kupandisha dau la straika wake wa Zambia, Felix Sunzu kuwa anauzwa dola 450,000 (Sh 800m) kutokana na kutokuwa na uhakika na wachezaji wanaotakiwa na Yanga. Bado kocha Kosta Papic hadi jana Jumatatu alikuwa hajawasilisha ripoti yake kwa uongozi, lakini Yanga ina nafasi za kusajili wachezaji wawili wazalendo kukamilisha usajili wa wachezaji 30. Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga ya Salum Rupia aliiambia Mwanaspoti kuwa; "Mambo mengi sana yanazungumzwa kuhusiana na usajili wa Yanga lakini naweza kukwambia mpaka sasa hakuna ukweli wowote, sisi ndio tunajua tunachokifanya na tunafanya kimyakimya sana." "Tuna mawasiliano ya karibu na benchi la ufundi na tunajua tufanye nini, usajili wetu hatutafanya kwa kukurupuka tunaenda taratibu na unaweza kushangaa tukakamilisha dakika za mwisho kabisa kwa kumchukua mchezaji ambaye hakuna ambaye angetarajia atatua kwetu. "Mipango yetu iko vizuri sana ndio maana hamsikii tukizungumza bila sababu,"alisema kiongozi huyo na kudai kuwa hawajafanya mazungumzo na Kelvin Yondani wa Simba kwa kuwa wanajua bado ana mkataba na timu hiyo. "Hakuna kilichofanyika kuhusiana na Yondani sisi tunajua ni mchezaji wa Simba, wala hajawahi kutangazwa kuachwa na sisi hatusajili bila kocha kusema,"alisisitiza Rupia. Papic ametangaza kufanya mabadiliko kadhaa kwa kuongeza wachezaji wa ndani kwenye kikosi chake nafasi muhimu aliyoisisitiza ikiwa ni beki wa kati ambayo Yondani wa Simba ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa sana. Yondani ana mkataba na Simba lakini amejiweka pembeni kwenye timu hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa hana uhusiano mzuri na uongozi wake. Lakini Papic akizungumza na Mwanaspoti jana Jumatatu, alisema nafasi ya beki wa kati ndio muhimu sana kuliko nafasi nyingine zozote. "Ni kama nilivyokwambia awali kuwa tutasajili wachezaji wawili au watatu, lakini nafasi ya beki wa kati ni muhimu zaidi kwa sasa." mwisho