Usajili mpya wanaotua England kabla ya Oktoba 5

Friday October 02 2020
usajil englnd pic

LONDON, ENGLAND. HARAKATI za usajili bado zinaendelea barani Ulaya, ikiwa zimebaki siku tatu kabla ya kufungwa Oktoba 5, klabu mbalimbali za Ligi Kuu England zinaonekana kuwa kwenye harakati za kufanya mazungumzo na klabu kadhaa ili kufanikisha usajili wa wachezaji ambao zinahitaji kuwatumia katika kwa msimu huu.

Kuna baadhi ya wachezaji ambao usajili wao unaonekana kuwa mbioni kukamilika na wanaweza kujiunga na klabu zinazowania saini zao katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Licha ya dirisha kufungwa Oktoba, 5, lakini klabu za Ligi Kuu, England zitaweza kusajili wachezaji kutoka ligi daraja la kwanza nchin humo hadi Oktoba, 16.

Mwanaspoti inakuletea orodha ya wachezaji ambao wanaweza kutua England ikiwa madili yao yanatarajiwa kukamilika kabla ya tarehe ya mwisho.

Jadon Sancho

Man United imekuwa inapambana  kuhakikisha inaipata saini ya mwamba huyu kwa muda mrefu ili kufanya maboresho katika safu yao ya ushambuliaji ambayo ineonakana kupwaya kwa zaidi ya misimu mitatu.

Advertisement

Borussia Dortmund inahitaji Pauni 108 milioni, ili kumuuza Sancho, lakini Man United inapinga na kuhitaji ipunguziwe bei jambo ambalo linaonekana kuwa ni gumu kukubaliwa.

Inaripotiwa, wawakilishi wa Man United na wa Jadon Sancho wameshafanya makubaliano na kinachosubiriwa ni kutolewa pesa kwa miamba hiyo ya Ujerumani.

Mapema wiki hii Dortmund iliripotiwa kukataa ofa ya Pauni 91.3 milioni iliyotolewa na Man United na kusisisitiza inahitaji Pauni 108 milioni.

Licha ya ofa hiyo kukataliwa Man United inasisitiza bado haijakata tamaa kwenye dili hilo na itapambana mpaka siku ya mwisho ya dirisha la usajili na inajipanga kuwasilisha ofa nyingine.

Houssem Aouar

Kiungo huyu wa Olympique Lyon amekuwa kwenye rada za Arsenal kwa muda mrefu, katika dirisha hili Arsenal iliwasilisha ofa ya Pauni 32 milioni ambayo ilikataliwa na baadae ikawasilisha nyingine ya Pauni 34.5 milioni ambayo iliukataliwa.

Lyon inaripotiwa kuhiataji kaisi cha Pauni 54 milioni kumuuza Aouar, 22, lakini haitokataa ikiwa kuna klabu itawasilisha ofa isiyopungua Pauni 45 milioni.

Dili la mchezzaji huyu linaripotiwa kuwa kwenye hatua za mwisho kukamilika kwa kuwa klabu hizo mbili zimekubaliana ada ya usajili  wa mwamba huyo ambaye msimu uliopita alifunga mabao tisa na kutoa asisti kumi baada ya kucheza mechi 40 za michuano yote.

Milan Skriniar

Tottenham Hotspur na Fulham zipo kwenye vita kali kuhakikisha zinaipata saini ya beki huyu wa kati wa Inter Milan.

Inter imeripotiwa kuwa ipo tayari kumuuza mwamba huyo kwa dau isilopungua Pauni 45 milioni, lakini Spurs imewasilisha ofa inayokadiriwa kuwa chini ya Pauni 35 milioni, huku Fulham ikiweka mezani Pauni 30 milioni, ikidhamiria kuvunja rekodi yao ya usajili ya Pauni 27 milioni.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, alionesha kiwango kikubwa katika msimu uliopita ambapo alicheza mechi 42 katika michuano yote na ikaiwezesha kufika fainali ya Europa League.

Declan Rice

Licha ya West Ham kutoa tamko la kutomuuza mchezaji huyo katika dirisha hili, lakini Chelsea bado inaamini inaweza kuipata saini yake.

Rice, 21, amekuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao kocha, Frank Lampard anahitaji kuwatumia kwenye mifumo yake kwa msimu huu ambao amesema anaijenga Chelsea mpya.

Mapema wiki hii Chelsea iliripotiwa kuwa kwenye mpango wa kutaka kuwasilisha ofa ya zaidi Pauni 40 milioni kwa West Ham, ikiamini itakuwa ngumu kwao kukataa kumuuza.

Dili la mwamba huyu ambaye msimu uliopita alicheza mechi 39 akafunga bao moja na kutoa asisti tatu, lakini alionesha uwezo mkubwa wa kufanya timu imiliki mpira na kuzuia timu pinzani kufanya mashambulizi katika lango lao.

Kurt Zouma

Chelsea imekuwa kwenye mpango wa kuwa miaka 25, alionesha kiwango kikubwa katika msimu uliopita ambapo alicheza mechi 42 katika michuano yote na ikaiwezesha kufika fainali ya Europa League.

Declan Rice

Licha ya West Ham kutoa tamko la kutomuuza mchezaji huyo katika dirisha hili, lakini Chelsea bado inaamini inaweza kuipata saini yake.

Rice, 21, amekuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao kocha, Frank Lampard anahitaji kuwatumia kwenye mifumo yake kwa msimu huu ambao amesema anaijenga Chelsea mpya.

Mapema wiki hii Chelsea iliripotiwa kuwa kwenye mpango wa kutaka kuwasilisha ofa ya zaidi Pauni 40 milioni kwa West Ham, ikiamini itakuwa ngumu kwao kukataa kumuuza.

Dili la mwamba huyu ambaye msimu uliopita alicheza mechi 39 akafunga bao moja na kutoa asisti tatu, lakini alionesha uwezo mkubwa wa kufanya timu imiliki mpira na kuzuia timu pinzani kufanya mashambulizi katika lango lao.

Kurt Zouma

Chelsea imekuwa kwenye mpango wa ku taka kumuuza  kwa dau lisilopungua Pauni 36 milioni, kabla ya dirisha hili kufungwa.

Zouma ambaye anacheza nafasi ya beki wa kati anauzwa kwa  sababu timu hiyo inataka kufidia Pauni 220 milioni ambayo iliitumia kufanyia usajili.

Everton ambayo iliwahi kupata huduma ya mchezaji huyo msimu wa 2018-19 ambapo alicheza kwa mkopo inatajwa kuwa kwenye harakati za kutaka kumsainisha lakini Leicester City nayo inaimezea mate huduma yake. Mkataba wa mwamba huyu umebakisha miaka mitatu.

Edinson Cavani

Kocha wa Manchester United katika kuhakikisha anaboresha safu yake ya ushambuliaji amekuwa kwenye mpango wa kutaka kumsajili mchezaji huyu wa zamani wa PSG ambaye ameachana nayo baada ya mkataba wake kumalizika mwisho wa msimu uliopita.

Cavani ambaye ana umri wa miaka 33, amefunga mabao 341 na kutoa asisti 65 tokea ameanza kucheza soka la ushindani hadi sasa.

 Mbali ya Cavani Man United pia imemuweka kwenye rada straika wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Serbia Luka Jovic ambaye Madrid imeweka wazi  kuwa  inahitaji kumuondoa hata kwa mkopo baada ya kushindwa kuonesha kiwango bora tokea aliposajiliwa kutoka Eintracht Frankfurt.

Ruben Loftus-Cheek

Aston Villa, West ham na Southampton  zipo kwenye hatua za mwisho kuhakikisha zinaipata saini ya mchezaji huyu kwa mkpo kutoka Chelsea ambayo inataka kumuondoa ili kupunguza gharama za uendeshaji wa timu baada ya msimu huu kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwenye masuala ya usajili.

Kocha wa Chelsea Frank Lampard hana mpango wa kumtumia mwamba huyo katika kikosi chake, hali inayosababisha Chelsea kuwa na mpango wa kutaka kumuondoa mchezaji huyo ambaye ameshindwa kuonesha kiwango bora tokea asajiliwe mwaka 2018 akitokea Crystal Palace.

 Ousmane Dembele

Manchester United ndio inaonekana kuwa kwenye hatua nzuri ya kuipata saini yake baada ya ripoti zilizotoka wiki hii kudai kuwa wawakilishi wao tayari wamewasili Jijini Barcelona  ili kukamilisha dili lake.

Barca inataka kumuuza  mchezaji huyo ili kupata pesa ya kumsainisha winga wa Olympique Lyon, Memphis Depay ambaye ni chaguo la kocha Ronald Koeman.

Mchezaji huyo hajaonesha kiwango kilichotarajiwa tokea asajiliwe Barcelona mwaka 2017 kwa ada ya Euro 133 milioni akitokea Borussia Dortmund na shida kubwa ni majeruhi ya mara kwa mara anayokumbana nayo.

Dili hilo huenda likakamilika kabla ya wiki hii kuisha na Man United itatakiwa kutoa kiasi kisichopungua Euro 60 milioni, Mkataba wa Dembele unatarajiwa kumalizika mwaka 2023 thamani yake katika soko la usajili ni Euro 56 milioni.

 

 

 

 

 

Advertisement