Ukata waitoa Mbeya Taifa Cup

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanasspoti Makamu wa Chama cha mchezo humo Mkoa wa Mbeya (MBA), Joseph Fyondi alikiri timu hiyo kujitoa kwenye mashindano hayo akieleza kuwa ukata ndio sababu.

WAKATI Ligi ya mchezo wa kikapu Taifa ‘Taifa Cup’ ikitarajia kuanza Juni 19, timu ya Wanaume mkoani Mbeya imejitoa kushiriki michuano hiyo ikidai kukabiliwa na ukata.

Akizungumza na Mwanasspoti Makamu wa Chama cha mchezo humo Mkoa wa Mbeya (MBA), Joseph Fyondi alikiri timu hiyo kujitoa kwenye mashindano hayo akieleza kuwa ukata ndio sababu.

Alisema licha ya maandalizi waliyokuwa wamfanya, lakini ahadi waliyokuwa wamepata kwa waliokuwa wadhamini wao, wamejitoa na kuwafanya kukosa nguvu ya kifedha kuweza kusafiri.

“Tayari tumeshawasilisha barua kwa uongozi Taifa kujitoa kwenye mashindano hayo, kikubwa ni fedha kwa sababu tulitarajia mdhamini wetu ila alijiondoa” alisema Fyondi.

Fyondi aliongeza kuwa kwa sasa nguvu yao itaelekezwa kwa timu ya Wanawake ambao wamepata ufadhili hivyo matarajio yao ni kuwa na uwakilishi mzuri na kubeba ubingwa.

Aliongeza baada ya mashindano ya Taifa, MBA itaanza mipango ya kuandaa ligi ya Mkoa na kwamba changamoto zilizojitokeza kuzifanyia kazi ili mwakani waweze kufanikisha.

“Tutawakilishwa na Wanawake katika mashindano hayo, lakini hii ni changamoto kwetu tutajipanga msimu ujao tusahihishe tulipokosea ili mwakani tuweze kushiriki kikamilifu” alisema kiongozi huyo.