Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uhamiaji FC yaachana na nyota saba!

UHAMIAJI Pict

Muktasari:

  • Hayo yamebainishwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdul Saleh Mohamed wakati akizungumza na Mwanaspoti.

WAKATI timu zikijiandaa na msimu ujao wa 2026-2027 kwa kuboresha vikosi vyao, Uhamiaji imeamua kuachana na wachezaji saba.

Hayo yamebainishwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdul Saleh Mohamed wakati akizungumza na Mwanaspoti.

Kocha huyo amesema wachezaji hao wapo ambao hawakuonesha kiwango kizuri, huku wengine uwezo wao umepungua.

Pia, amesema wapo wachezaji ambao walisajiliwa msimu wa 2025-2026 kwa lengo la kuisaidia timu, lakini kwa bahati mbaya hawakufikia malengo.

“Timu ina mpango wa kuacha wachezaji kama saba kwasababu wamepungua viwango na wengine tulikuwa nao hawajatuonesha kile ambacho tulikitaka ndani ya uwanja,” amesema.

Mbali na hilo, kocha huyo, amesema katika kuboresha kikosi hicho watafanya usajili wa beki wa kati na mshambuliaji kwani hayo ndio maeneo ambayo hayapo vizuri.

Uhamiaji ni miongoni mwa timu zilizoanza vizuri msimu wa 2025-2026 kwa kushika nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar, lakini ilimaliza msimu nafasi ya tano baada ya kusuasua ikiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 30, ikishinda 15, sare sita na kupoteza 10 huku ikifunga mabao 46 na kuruhusu 27.