Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ufunguzi umiseta, umishumta wanoga

UFUNGUZI wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na taaluma kwa shule za msingi na sekondari jana Jumanne yalizinduliwa kwa kishindo na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa mjini hapa.

Majaliwa aliwapongeza wanafunzi kwa kuonyesha vipaji katika fani mbalimbali na kuchaguliwa kushiriki fainali hizo na kuwasihi kuonyesha uwezo wao kwa nidhamu ya hali ya juu na kuiletea mafanikio mikoa yao.

“Nawapongeza walimu kwa kazi yao nzuri wanayoifanya ya kufundisha kwa moyo na kufanya kazi kwa bidii.”

Kauli mbiu ya michezo ya mwaka huu inasema ‘Michezo, Sanaa na Taaluma kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda’ inasadifu kwa kiasi kikubwa nia ya Serikali na chama Tawala, kutumia kila fursa tuliyo nayo kuleta maendeleo ya wananchi wetu na taifa kwa jumla.

“Kaulimbiu ya mwaka huu inaelezea uhusiano na nafasi kubwa iliyopo ya Michezo, Sanaa na Taaluma katika ujenzi wa uchumi wa Taifa. Kauli mbiu hii inamtaka mwanafunzi afahamu na kuelewa kuwa katika masomo yake anatakiwa pia aandaliwe na kuhimizwa kujihusisha na kushiriki michezo na sanaa kama sehemu muhimu za taaluma,”anasema

Majaliwa kwenye hotuba yake aliongeza; “Tunalalamika sana wanamichezo wetu hawafanyi vizuri michezo ya Kimataifa. Tunapaswa tukae chini na kujiuliza, Je tunawaandaa wanamichezo wetu inavyostahili. Jibu ni hapana. Hatujafanya jitihada za kutosha kuandaa watoto wetu kulitumikia taifa kwa uwezo wao wote.

Hatujaweza kuwawekea mazingira rafiki katika kutambua, kukuza na kuendeleza vipaji kimkakati ili kuchangia katika maendeleo ya uchumi wa taifa.

“Sasa Serikali imeamua kulisimamia suala hili kikamilifu. Rais ameshatoa maelekezo ya kuiangalia mitaala ya Elimu ijielekeze kujenga stadi za ujuzi kwa maendeleo ya Taifa. Stadi hizo na pamoja na Elimu kwa Michezo na Sanaa. “Matokeo bora ya kujenga uchumi wa viwanda yanategemea sana nguvu kazi bora. Nguvu kazi bora ni ile iliyoandaliwa vizuri katika ngazi zote kuanzia umri wa shule za awali, shule za msingi, sekondari na vyuoni. Maandalizi hayo ni lazima yawe na muunganiko kutoka ngazi moja kwenda nyingine ili uweze kupata matokeo bora.

“Kupata wanamichezo na wasanii chipukizi wengi na bora, hatuna budi kuimarisha ufundishaji wa taaluma hizo kuanzia ngazi za awali, msingi, sekondari na vyuo. Kila ngazi ina umuhimu na kujenga msingi wa ngazi inayofuatia.

“Ndiyo sababu katika nchi zilizoendelea wanamichezo wake wengi wanaoshiriki michezo ya Kimataifa kama vile Olimpiki na Jumuia ya Madola ni wanafunzi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu.

“Tanzania tunayo hazina ambayo tukiitumia kikamilifu, tunaweza kufanya vizuri katika michezo na uchumi wa taifa kwa jumla. Nimefurahi kusikia kuwa mwezi huu wataajiriwa angalau walimu wachache kwa shule za msingi.

“Nisisitize tena, Wizara zote husika zikae chini kuingalia Mitaala iliyopo kama inakidhi mahitaji ya sasa na kuchukua hatua stahiki pale ambapo kutaonekana kuna upungufu.

“Ufundishaji wa somo la elimu kwa michezo ufanyike kwa wanafunzi wote na madarasa yote shule za msingi na kutoa fursa na kuhamasisha wanafunzi wa shule za sekondari kusoma somo hilo.

Hatua hiyo, siyo tu ituwekea misingi imara kwa wanamichezo wetu, itasaidia kupata manufaa mengine kwa watoto wetu kama vile kujenga moyo wa kujiamini, ubunifu, mshikamano na umoja wa kitaifa na kuimarisha afya ya taifa. “Nahimiza wito wa Rais Samia Suluhu Hassan, aliotoa kuwahimiza wananchi kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukizwa yanayotokana na mtindo wa maisha tunayoishi.

Magonjwa haya yanawagharimu wahusika fedha nyingi katika matibabu na tuendelee kuunda vikundi vya mazoezi ya ukakamavu (Jogging na matamasha mbalimbali ya michezo) na kimsingi kujijengea utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara kwa afya zenu.

“Mwisho, nawaasa vijana mjiepushe na vitendo vitakavyokwamisha ndoto zenu za kufanikiwa masomo na michezo kama vile matumizi ya dawa ya kulevya, uvivu na utoro shuleni. Tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu aendelee kutupa afya njema, tukae mahali hapa kwa amani, tucheze na kumaliza michezo yetu kama ilivyopangwa na hatimaye tuweze kurejea nyumbani salama,” anasema Majaliwa.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa kwenye hotuba yake ya ufunguzi alisema;

“Tumealika watalaam wa kuvumbua vipaji, kutoka Taasisi ya Mbwana Samata, pamoja na watalaamu kutoka Sweden ili kuja kuvumbua vipaji.”

“Wizara katika kutimiza malengo yake inatarajia kuanzisha kituo maalum cha kuendelezea michezo (Center of Sports Excellency), katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya ili kuendeleza vipaji vinavyopatikana,” anaongeza Bashungwa.

Kwa upande wa Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, David Silinde kwenye hotuba yake alisisitiza malengo makuu ya kuendeleza mashindano hayo ni pamoja na kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya sita ya kukuza vipaji vya michezo kwa kuibua na kuendeleza vipaji.