UDSM yaoimba CCCC kuwajengea uwanja wa mpira

Kampuni ya ujenzi ya China Communications Construction Company (CCCC), imeombwa kuwajengea uwanja wa mpira chuo kikuu cha Dar es Salaam jambo litakaposaidia kuongeza  shughuli za Utamaduni kwa  kujumuisha michezo

Ombi hilo lilitolewa na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shahada za Uzamili UDSM, Profesa Donatha Tibuhwa wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba mashirikiano na chuo hicho ya kutoa ufadhili kwa wanafunzi kwa ajili ya mafunzo ya vitendo katika kampuni hiyo yenye makao yake makuu nchini China.

Kampuni ya CCCC, ndiyo iliyohusika na ujenzi wa maktaba ya kisasa  chuo hapo, iliyogharimu kiasi cha Sh90 bilioni, ikiwa ina uwezo wa kuchukua watu 2,100 kwa wakati mmoja.

Akizungumza katika hafla hiyo, Profesa Donatha, wana kila sababu ya kujivunia mkataba hiyo ambayo sio kubwa tu nchini bali na kwa nchi za Afrika Mashariki.

“Ni kutokana na kujivunia makataba hiyo, leo tunarudi tena kuwaomba mtujengee uwanja wa mpira ambao mbali ya kukuza afya za wanafunzi pia utawapa wa fursa ya kufaulu katika michezo.

Jingine amesema uwanja huo utasaidia kufungua njia zaidi kwa shughuli za kitamaduni za Wachina, na kusimama kama ushuhuda mwingine wa kudumu wa urafiki wa muda mrefu.