Tukitathimini ya mwaka 2018,tujipange 2019
Muktasari:
Mwaka 1992 ukitajwa na Manchester United unaamisha watu sita ambao ni David Beckham, Nicky Butt, Ryan Giggs, Gary Neville, Phil Neville na Paul Scholes.
Ni dalili ya kuwa na heri na baraka kwetu sote ambao leo hii tumepata nafasi ya kupitia makala hii ikiwa ni jumamosi ya kwanza ndani ya mwezi wa kwanza wa mwaka 2019 wakati wapo wenzetu wengi tunaowafahamu na tusiowafahamu ambao tulikuwa nao mwaka uliopita lakini kwa mapenzi ya Mungu hawakupata bahati ya kuuona mwaka huu ambao kwa mujibu wa kalenda tunayoitumia ya Gregori (Gregorian calendar) ni mwaka 2019.
Kwa kuwa kutoka mwaka mmoja kwenda na kufika mwaka mwingine ni mafanikio katika maisha hivyo ni kawaida kwa mwanadamu kuyafurahia mafanikio ingawa yapo mafanikio ambayo mwanadanu anaweza kujivunia kutokana na mchango wake katika kuyafikia mafanikio hayo lakini yapo mafanikio mengine ambayo manadamu hawezi kujivunia kutokana nakutokuwa na mchango wowote katika kuyafikia mafanikio hayo. Miongoni mwa mafanikio ambayo mwanadamu huwa hana mchango wake ni hiki ninachokizungumzia hapa yaani ni kufanikiwa kuwa hai na afya njema kama hivi tulivyo leo huku tukiwa tunapata makala ya kwanza kabisa kwa mwaka huu tukiwa salama.
Kwa kadiri miaka inavyozidi kusonga mbele ndio watu huweza kujitathmini viwango vya maendeleo katika mambo wanayoyafanya katika maeneo yao ya kazi ndio maana ukiona mtu anasherehekea kuuaga au kuukaribisha mwaka fulani basi ujue mtu huyo ana kitu cha kijuvunia katika mwaka huo.Ndio maana ukienda katika kumbukumbu za historia za timu ya Manchester United ya nchini Uingereza utasikia pamoja na mafanikio waliyoyapata lakini lazima wanataja darasa la mwaka 1992 (Class of 1992). Sababu gani mwaka huo unatajwa ? tu kwa sababu ndio mwaka vijana sita walifaulu kutoka katika timu ya vijana na kujiunga na kikosi hicho ambacho kilipata mafanikio makubwa kwa kutwaa vikombe vitatu katika msimu wa mwaka 1998/1999. Hivyo mwaka 1992 ukitajwa na Manchester United unaamisha watu sita ambao ni David Beckham, Nicky Butt, Ryan Giggs, Gary Neville, Phil Neville na Paul Scholes.
Kufanya tathmini kila mwaka unapoisha ni moja kati ya kitu kinachotakiwa kufanyika kuanzia ngazi ya wachezaji, makocha, vingozi na baadae washabiki kwani kila mmoja ana nafas I yake katik aeneo lake itakayoweza kumfanya akumbukwe hata kama hatakuwepo. Leo hii tumekuwa tukimtaja Peter Tino kwa kuwa ndiye aliyefunga goli dhidi ya Zambia lililotupeleka Tanzania katika Fainali za Mataifa huru ya Afrika za mwaka 1980 zilizofanyika nchini Nigeria.
Naandika kuwa jamii ya wanasoka Tanzia inatakiwa kutahmii kile tulichokifanya katika mchezo huu ili tuweze kujirekebisha mwka unaofuata kwani mwaka huu 2019 tunatarajia kuwa wenyeji wa fainali za CAF za vijana wenye umri chini ya miaka 17 hivyo kuitumia fursa hiyo kuandika historia itakayokumbukwa na vizazi vijavyo. Lakini kuweka historia huwa hakuji hivi hivi bali huhitaji maandalizi ambayo hufanyika baada ya kujitathmini kama ambavyo tunatakiwa kuutathmini mwaka 2018 na soka la Tanzania.Miongoni mwa mafanikio ya mwaka 2018 ni timu yetu ya soka Taifa U-17 kushika nafasi ya pili katika mashindano ya U-17 katika ukanda wa nchi za cecafa nyuma ya Uganda ambayo ilitwa ubingwa, timu hiyo hiyo ilitwaa , timu hiyo hiyo ya Vijana U-17 ilitwaa ubingwa wa mashindano hayo ya vijana kwa nchi za COSAFA ambayo iliakikwa katika mashndano hayo. Kwa upande wa vilabu ni Simba kufanikiwa kuingia ktika hatua ya makundi kwenye michunaoi vya vilabu bingw abarabni Afrika.
Kwa upande wa pili ambao unatakiwa kuangaliwa kwa makini na kutafuta kilichosababisha ni kuwa mwaka 2018 ndio mwaka timu yetu ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 ilitolewa katika masindano ya CAF kwa vijana wenye umri huo, timu yetu ya Taifa ya wakubwa ilipoteza matumaini ya kushirii katika fainali za CAF za mwaka huu baada ya kupoteza mechi dhidi ya lesotho ambayo ilionekana kuwa na wepesi wa kupata matokeo ukilinganisha na timu nyingine atika kundi letu. Lakaini pia mwaka 2018 ndio mwaka ambao ligi kubwa kabisa nchini ya soka yaani ligi kuu ilimaliza mkataba wa udhamini na mdhamini mkuu hivyo ligi hiyo kuchezwa bila y kuw an mdamini mkuu. Hivyo ni imani yangu kuwa wadau wote tuliopo katka mchezo wa soka kila mtu akijifanyia tahmini yake katika eneo linalomhusu kwa kuungalia mwaka 2018 kisha akajipanga kwa ajili ya mwaka huu 2019 naamini yatakuwa ni mafanikio makubwa sana kwa ujumla wake hapo mbeleni!
Kwa leo naishi hapo huku nikisubiri mrejesho kutoka kwako.